February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Hospitali zote zatakiwa kuonesha vipindi vya Afya

Spread the love

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya , Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wafawidhi kuonesha vipindi vya Afya kwenye luninga zote zinazoweka kwenye mahospitali nchini. Anaripoti Abdallah Khalifa … (endelea).

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile wakati wa ziara yake ya kujua hali ya upatikanaji wa huduma za Afya katika Hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma.

“Marufuku kwa Hospitali na sehemu yoyote ya kutolea huduma za afya kuonesha vipindi vingine tofauti ikiwemo miziki, mpira , na vipindi vya wanyama na badala yake Luninga zote ziwekwe vipindi vya kuelimisha juu ya magonjwa yasiyo ya kuambikiza na yale ya kuambukiza ili waweze kujikinga,” alisema Dk. Ndugulile

Aidha Dk. Ndugulile amewataka wananchi hususan wakazi wa Dodoma kujitokeza kwenda kupata vipimo vya kundua saratani ya matiti kwani huduma hiyo inapatikana katika Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa ufanisi.

Dk. Ndugulile amesisitiza kwamba Hospitali ya Benjamini Mkapa kwa sasa ipo vizuri kutoa huduma bora za Afya na kujenga wodi mpya zenye uwezo wa kulaza wagonjwa zaidi ya 400 na kuongeza watumishi zaidi ya 100.

Mbali na hayo Dk. Ndugulile aamesema kuwa Wizara imedhamiria kuboresha huduma za Afya ili ziweze kupatikana kwa kiwango na ubora unaotakiwa kutolewa kwa wananchi wote nchini.

Kwa upande wake Mkurigenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dk. Alphonce Chandika amesema kuwa Wananchi wanakaribishwa Hospitalini hapo kupata huduma bora kwani wamejidhatiti kutoa matibabu ya kibingwa nchini na nje ya nchi.

“Tumeboresha majengo, wodi, vifaa na vifaa tiba hivyo tupo tayari wakati wote kutoa huduma bora za afya kwa wananchi hapa Tanzania na nchi jirani katika kutoa huduma za matibabu ya kibingwa,” alisema Dk. Chandika

MWISHO

error: Content is protected !!