October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hospitali zaagizwa kuanzisha ‘mfuko wa fedha za dawa’

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akikata utepe ishara ya uzinduzi wa Bodi mpya ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou-Toure

Spread the love

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, imeagiza Waganga Wakuu wa Vituo vya Afya na Hospitali zote nchini, kuanzisha mfuko wa fedha za dawa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amesema, mfuko huo upitie makusanyo ya fedha za ndani, ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa dawa nchini endapo itatokea.

Kauli hiyo imetolewa na Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kikao cha uzinduzi wa bodi mpya ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza.

“Kuanzia Vituo vya Afya, Hospitali zote za Halmashauri, za Mikoa, kuanzisha mfuko wa fedha za dawa, na vyanzo vikuu vya mifuko hii ni mapato yatokanayo na mauzo ya dawa, huduma za Maabara, huduma za mionzi” alisema Waziri Ummy.

Amesema, bodi hiyo ya ushauri lengo lake ni kuhakikisha inaboresha huduma za kinga na tiba katika hospitali na kufikisha huduma hizo kwa ubora na gharama nafua.

Waziri Ummy amesema, sera ya afya nchini inawataka wananchi kuchangia huduma kwa gharama nafuu, isipokuwa kwa makundi yote ya msamaha wakiwemo wazee, watoto walio chini ya miaka mitano na mama wajawazito.

Mbali na hayo, Waziri Ummy ameiagiza bodi hiyo kuhakikisha inaboresha huduma za dharura na ajali, ili kuokoa vifo vitokanavyo weza kuepukika kupitia huduma za dharura, keisha kuwashauri kujenga jengo jipya la wagonjwa wa nje (OPD) ili kuboresha huduma kwa wananchi.

“Watu wengi wanakufa wakiwa getini Mwa Hospitali, wakati utaalamu upo, kwamba mkiboresha huduma za dharura na ajari, tunaweza kuokoa maisha ya watu wengi ” alisema Waziri Ummy.

Aidha, ameeleza majukumu ya bodi hiyo ni kushauri, kutengeneza, kusimamia na kupitisha miongozo, malengo na mipango mikakati ya Hospitali kulingana na Sera na miongozo ya Serikali.

Dk. Graham Mtui, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekou-Toure, ameishukuru serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuendelea kuboresha huduma za afya katika hospitali, hiyo kwa kuwapatia mashine ya uchunguzi wa figo na ini, mashine ya kusafisha figo ambazo zinatarajia kuanza kutoa huduma Januari 2020.

Amesema, hospitali inatarajia kupokea mashine sita ikiwemo CT Scan, X- ray yakidigitali, vifaa vya mifupa na mashine zinazosaidia kupumulia kutoka Bohari ya Dawa (MSD).

Hata hivyo, amesema kuwa, idadi ya Wagonjwa wanaofika kupata huduma, kutoka wastani wa wagonjwa 350 kwa siku kwa mwaka 2015 hadi kufikia wagonjwa kati ya 500 mpaka 700 kwa Mwaka huu 2019, huku akiweka wazi kupunguza Rufaa za kwenda Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Bugando kwa asilimia 50.

“Kutokana na mafanikio hayo, idadi ya wagonjwa wanaopata huduma katika Hospitali imeongezeka, kutoka wastani wa wagonjwa 350 kwa siku ambayo ilikuwa mwaka 2015, na kufikia wastani wa wagonjwa kati ya 500 hadi 700 kwa mwaka huu 2019”, alisema Dk. Graham Mtui.

error: Content is protected !!