Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Hospitali yashambuliwa Darfur
Kimataifa

Hospitali yashambuliwa Darfur

Spread the love

 

SHIRIKA la misaada ya kimatibabu la madaktari wasio na mipaka (MSF) linasema kuwa watu watatu wameuawa ndani ya hospitali katika eneo la Kreneik huko Darfur nchini Sudani. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo, limesema kuwa hospitali imeshambuliwa na duka la dawa la hospitali hiyo, liliporwa pamoja na waathiriwa wa tukio hilo ni wafanyakazi wawili wa matibabu .Timu za MSF hawakuwepo kwenye kituo hicho wakati wa shambulio hilo ,shirika la misaada liliongeza.

MSF inasema kuwa uvamizi wa pili, ulifanyika katika Hospitali ya Mafunzo ya EI Geneina katika mji mkuu wa Darfur Magharibi ,huku ufyatuaji wa risasi ukifanyika ndani ya kituo hicho,ikiwa ni Pamoja na chumba cha dharura.

Hata hivyo mfanyakazi mmoja wa hospitali aliuawa, na wafanyakazi wa afya wakiwemo wale wa MSF, ’’Tumeshtushwa na mashambulizi haya tunatuma rambirambi zetu za dhati kwa familia zilizoathiriwa na tukio hilo.’’

“Tunalaani uvamizi huo mbaya kwa maneno makali iwezekanavyo,’’ ilisema taarifa hiyo, Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kufanya uchunguzi kuhusu mapigano katika siku za hivi karibuni kati ya jamii ambayo ililipotiwa kusambaza vifo vya zaidi ya watu 160.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!