Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari Hospitali yakanusha madai maiti ya msanii kuimba Ekwueme usiku
HabariKimataifa

Hospitali yakanusha madai maiti ya msanii kuimba Ekwueme usiku

Spread the love

HOSPITALI ya Kitaifa ya Abuja nchi Nigeria imekanusha madai kuwa maiti ya mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili, Osinachi Nwachukwu, ilikuwa ikiimba ‘Ekwueme’ katika chumba cha kuhifadhi maiti. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Msemaji wa hospitali hiyo, Dk. Taiwo Haastrup jana tarehe 17 Mei, 2022 amesema hakuna uthibitisho kwamba mwili wa Osinachi ulikuwa ukiimba katika chumba cha kuhifadhi maiti.

Akizungumza na waandishi wa habari Haastrup amebainisha kuwa mtu aliyekufa hawezi kuimba akiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.

Osinachi ambaye alikuwa mwanakwaya katika Kanisa la Kimataifa la Dunamis, alifariki miezi michache iliyopita kutokana na kile kinachosemekana kuwa unyanyasaji wa nyumbani aliofanyiwa na mumewe, Peter Nwachukwu.

Kufuatia kifo chake, mwili wake ulihifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Taifa.

Ripoti zilienea kwamba wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti walidai kuwa maiti ya Osinachi ilikuwa ikiimba wimbo wake wa ‘Ekwueme’, usiku wa manane.

Akijibu ripoti hiyo, Haastrup alisema: “Kitabibu hakuna kitu kama hicho; ni mawazo ya watu tu. Mtu ambaye amekufa atawezaje usiku?.

“Hakuna kielelezo cha matibabu kwa hilo; ni mawazo ambayo yanaweza kuwa ni kutokana na kanisa alilohudhuria akiwa hai, na umaarufu wa nyimbo zake ndizo zinaweza kuwapa watu mawazo ya aina hiyo, lakini hakuna uthibitisho kwa njia yoyote,” amesema.

Kuhusu ripoti ya uchunguzi wa maiti, Hasstrup amesema: “Ni kesi ya uchunguzi, na ni siri; hatuwezi kufichua chochote hapo. Anayehusika kuchunguza atampa ripoti Mkuu wa Jeshi la Polisi ambaye atapeleka mahakamani,” amesema.

Hata hivyo, ripoti ya uchunguzi wa tukio mwili wa msanii huyo tayari imewasilishwa polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!