June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hospitali ya Sekou Toure yashtakiwa kwa Rais Magufuli

Spread the love

HOSPITALI ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure inakabiliwa na changamoto lukuki zikiwamo za ubovu wa mashine za Ultra Sound na ile ya kutambua magonjwa (CD4) kuharibika huku haifahamiki zitatengenezwa lini. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Hayo yalibainika juzi wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, alitembelea hospitali hiyo kwa lengo la kuzungumza na wagonjwa, watumishi na menejimeti ya Sekou Toure juu ya changamoto zinazowakabili.

Mulongo ambaye aliwasili katika hospitali hiyo saa 5:11 asubuhi, akiongozana na viongozi wengine kutoka mkoani, ambapo alipofika mapokezi alijionea wagonjwa wakiwa wamepanga mstari kila kona kupata huduma.

Hata hivyo baada ya Mulongo kufika katika eneo hilo, wagonjwa waliokuwa katika eneo hilo, walianza kulalamika huku wengine wakiwatuhumu watumishi wa hospitali hiyo kwamba wamekuwa ni wazembe wakupindukia.

Mmoja wa wagonjwa hao akitoa malalamiko yake kwa Mulongo, Festo Kagaruki, amesema wagonjwa wanaopofika hospitalini hapo hawapati huduma kwa wakati kitendo kinachohatarisha uhai wa binadamu, hivyo Serikali inapaswa kuangalia tatizo hilo.

Pia baada ya Mulongo kuzungumza na wagonjwa hao ambao wengine walidai walifika hospitalini hapo tangu saa 12 asubuhi, alikwenda kutembelea baadhi ya idara na vitengo mbalimbali ambapo alipofika kwenye idara ya utambuzi wa magonjwa (CD4) alikuta mashine hazifanyi kazi.

Hata hivyo baada kujionea hali hiyo, Mulongo aliulizwa uongozi wa hospitali hiyo ni kwanini mashine hizo hazifanyi kazi, ambako Katibu wa Hospitali hiyo, Danny Tembo, alidai kwamba kampuni ya Phillips, muda wote itakwenda kuzitengeneza.

Hata hivyo baada ya majibu hayo ya katibu kutolewa, Mulongo alitaka kupewa namba za wataalamu wanaokuja kutengeneza mashine hizo, ambapo katibu Tembo alitoa namba za meneja wa Phillips ambaye hata hivyo alipopigiwa alikana kuhusika na matengenezo.

Kufuatia hatua hizo Mkuu huyo wa Mkoa, Magesa Mulongo, alitoa siku tatu kuanzia jana kuhakikisha kwamba mashine zote ambazo hazifanyi kazi kuhakikisha zinafanya pamoja na kujengwa duka la Serikali hospitalini hapo.

“Hizo siku nilizotoa zikifika tu, mashine zote ambazo hazifanyi kazi ziwe zimetengenezwa, pia angalieni utaratibu wa kuwahudumia wagonjwa wanaokuja hapa, haiwezekani mgonjwa tangu sa 12 asubuhi hajahudumiwa,” amesema Mulongo.

Katibu wa Hospitali hiyo, Danny Tembo, baada ya kupewa agizo hilo, alimhakikishia Mkuu wa mkoa, kwamba siku zilizotolewa mashine zote ambazo hazifanyi kazi zitakuwa zimetengenzwa tayari kwa huduma.

error: Content is protected !!