July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hospitali ya Lugalo yapigiwa chapuo

Mbunge wa Viti Maalum, Maryam Salum Msabaha

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Maryam Salum Msabaha (Chadema) ameitaka serikali kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya kukarabati majengo ya Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na kupata vifaa vipya vya kutendea kazi. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Ushauri huo umetolewa leo bungeni na mbunge huyo kwa maelezo kuwa, baadhi ya majengo ya hospitali hiyo yamechakaa pia baadhi ya vitendea kazi pia vimechakaa.

Akiuliza swali la msingi, alitaka kuelewa ni lini serikali itatoa fedha za kutosha ili kukarabati majengo na kupata vifaa vipya vya kutendea kazi.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi amesema, majengo na vifaa tiba katika Vituo vya Tiba vya JWTZ ikiwemo Hospitali ya Jeshi la Lugalo yamekuwa yakifanyiwa ukarabati na kununuliwa vifaa tiba mara kwa mara kwa kutumia fedha ambazo serikali imekuwa ikitoa kila mwaka.

Amesema, Julai, 2013 serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ilitoa Sh. Milioni 161 kwa ajili ya ununuzi wa mashine mpya ya kisasa ya X-ray aina ya Digitali pamoja na vifaa mbalimbali vya upasuaji.

error: Content is protected !!