January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hospitali ya Apollo yaendesha kambi ya moyo

Moyo wa binadamu

Spread the love

MACHI mwaka huu, sekta ya afya Tanzania imepokea wataalam kutoka nchi  mbalimbali duniani kwa ajili ya kutoa huduma za vipimo, ushauri na matibabu kwa watanzania. Anaandika Mwandishi wetu … (endelea).

Ujio huu umeleta faida kubwa kwa wagonjwa na wataalamu nchini. Miongoni mwa waliotembelea ni timu ya madaktari bingwa kutoka Israel na Hospitali za Apollo zilizopo nchini India.

Ziara hizi za mwishoni mwa Machi, zilitanguliwa na ziara ya madaktari wawill kutoka hospitali ya Apollo ya Bangarole mwanzoni mwa mwaka huu.

Pamoja na kufanya kliniki ya ushauri kwa ajili ya wagonjwa wa figo na mfumo wa fahamu, timu ya wataalam kutoka hospitali ya Apollo Bangalore ilirudi Tanzania kwa ajili ya uchunguzi na kutoa ushauri zaidi kwa wagonjwa wa moyo na mfumo wa fahamu.

Kliniki hiyo ilifanyika mwishoni mwa Machi katika hospitali ya Medi Ed jijini Dar es salaam na kuandaliwa na Dk. Girish Navasundi- dakitari mwandamizi wa magonjwa ya moyo, katika hospitali ya Apollo ya Bangalore na Prof. Krishna Kambadoor- Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi ya mfumo wa fahamu kutoka hospitali ya Apollo ya Bangalore.

Kliniki hiyo ilitoa fursa kwa umma kupata uchunguzi wa matatizo hayo bure na pia kuruhusu madaktari kufuatilia maendeleo ya wagonjwa wao ambao hawakuweza kurudi India kwa uchunguzi na matibabu ya zaidi.

Magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NCD)  kama vile moyo, mfumo wa neva na mgongo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi na kusababisha  ongezeko la vifo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati madaktari kutoka Israel wakiwafanyia uchunguzi watoto wenye matatizo ya moyo, Makamu wa Rais wa Chama cha Madaktari wa Watoto Tanzania, Dk. Namala Mkopi, alizungumzia matatizo ya magonjwa ya moyo kwa jamii na hasa kuonyesha athari zake kwa watoto wachanga.

Amesema “inakadiliwa watoto 13,600 nchini huzaliwa na  matatizo ya moyo kila mwaka na asilimia 25 tu ndio wana uwezo wa kupata matibabu. Mwaka 2013 na 2014 kati ya watoto 322 waliokutwa na matatizo, 128 tu walipata nafasi ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi.”

Wakati wa wakati wa kambi ya uchunguzi iliyooandaliwa na  hospitali ya Apollo, Dk. Girish Navasundi- mwandamizi wa magonjwa ya moyo, aliwahudumia wangonjwa wenye magonjwa yanayohusiana na moyo.

error: Content is protected !!