Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Maisha Afya Hospitali Kuu ya Jeshi la Polisi yanufaika na mafunzo kutoka Marekani
AfyaHabari Mchanganyiko

Hospitali Kuu ya Jeshi la Polisi yanufaika na mafunzo kutoka Marekani

Spread the love

 

HOSPITALI Kuu ya Jeshi la Polisi iliyopo wilaya ya Temeke Barabara ya Kilwa Mkoa wa Dar es Salaam itanufanika na mafunzo ambayo yatatolewa kwa muda wa siku mbili na shirika la Quality heathcare Solution and Consulting (QHSC) ambalo lina husika nakutoa mafunzo kwa watoa huduma za afya makazini ili kuwajengea uwezo madaktari kutoa huduma bora katika hospital hiyo. Anaripoti Abel Paul wa Jeshi la Polisi, Dar es Salaam … (endelea).

Akiongea mara baada ya mafunzo kwa Madaktari na wauguzi kutoka hospital kuu ya Jeshi la Polisi Dk. Harrieth Kokushubila Gabone ambaye ni Rais wa shirika hilo amesema wamefika katika hosptali hiyo kwa lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kuwasaidia wananchi wenye magonjwa ya moyo wanaofika kupata huduma katika hospital hiyo.

Ameongeza kuwa wamefika hapo na wataalam kutoka marekani na watatoa mafunzo kwa muda wa siku mbili ambayo yamelenga kuwajengea mbinu ya namna ya kuokoa Maisha ya wananchi wenye changamoto ya magonjwa ya moyo.

Kwa upande wake Daktari mfawidhi wa hospital kuu ya Jeshi la Polisi Dk.Nyanda Lushina amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kufanikisha kuwaleta wataalam hao katika hosptali hiyo ambapo amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo Mkubwa kiutendaji.

Nae Mrakibu mwandamizi wa Polisi, SSP Emmanuel Shija ameshukuru shirika hilo kutoka marekani kwa kutoa elimu ambayo amebainisha kuwa elimu hiyo imekuja wakati muafaka kwao kwani wamekuwa wakipokea wagonjwa wenye changamoto ya magonjwa ya moyo.

Pia Konstable wa Polisi Daktari Davis Mwita kutoka kitengo cha dharura Hospital kuu ya Jeshi la Polisi amebainisha kuwa mafunzo hayo yamewaongezea ujuzi na maarifa watakayo yatumia pindi wanapotoa huduma kwa askari Pamoja na wananchi wengine wanaofika katika hosptali hiyo kupata huduma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

error: Content is protected !!