Tuesday , 27 February 2024
Home Kitengo Maisha Afya Hospitali binafsi kugharamia damu salama
Afya

Hospitali binafsi kugharamia damu salama

Spread the love

MPANGO wa Taifa wa Damu salama imetakiwa kuhakikisha Hospitali Binafsi zote zinaanza kuchangia gharama za huduma za afya ili kupata mgao wa damu. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile wakati alipofanya ziara ya kukagua mashine za kupima sampuli za damu na utendaji kazi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama.

Katika ziara hiyo Dk. Ndugulile amesema kuwa ni lazima Mpango huyo uhakikishe unajiendesha wenyewe na kuhakikisha unapunguza gharama za utegemezi kwa Wafadhili na Serikali katika kutimiza majukumu yake.

“Ni lazima kupunguza gharama za utegemezi kwa Wafadhili na Serikali kwa kuanzisha mfumo wa uchangiaji gharama za huduma za Afya wakati Sera inaelekea kukamilika, Mpango unapendekeza kurudisha gharama kutoka Hospitali binafsi kupitia njia ya Bima,” alisema Dk. Ndugulile.

Dk. Ndugulile alisema kuwa Idadi kubwa ya wanaokuja kuchukua Damu katika Taasisi hiyo ni Hospitali Binafsi ukilinganisha na Hospitali za Umma, ambapo mfumo wake ni wakutoza huduma kwa Wananchi (Biashara)

“Wanaokuja kuchukua Damu nyingi hapa, wengi ni Hospitali Binafsi, kuliko hata za kwetu za umma, Damu nyingi tunawapa, lakini hawa tukiwapa Damu hizi, wao wanaenda wanatoza pesa, kwahiyo sisi tunawatengenezea bidhaa bure halafu wao wanaenda kutoza pesa, hata senti tano sisi hatupati, sio sahihi,” alisema Dk. Ndugulile.

Aidha, Dk. Ndugulile amewaagiza viongozi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuangalia ni namna gani Damu iwe ni moja ya vitu vitakavyo gharamiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

“Muwahusishe Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kuangalia jinsi gani damu itakuwa inagharamiwa na Bima ya Afya, mtuletee mapendekezo na sisi tutafanya maamuzi,” alisema Dk. Ndugulile.

Mbali na hayo Dk. Ndugulile ameagiza kufanya maboresho ya mfumo wa Takwimu kuanzia kwenye ukusanyaji wa mapato mpaka hatua ambayo mgonjwa anapata damu hiyo jambo litakalosaidia kuboresha huduma kwa wananchi.

Kwa upande mwingine Dk. Ndugulile ameagiza kuweka mikakati ya kuhakikisha wanawabakishia wachangiaji Damu ambao wanakuja kuchangia, hii inatokana na takwimu kuonesha Wachangiaji wa Damu wa hiari wanapungua kutoka 67% mpaka 63% mwaka 2017-18.

“Taarifa yenu ya Mwaka 2017-18 inaonesha kwamba, wachangiaji Damu wa hiari wanapungua kutoka 67% mpaka 63% , maana yake bado kuna changamoto, na kuna kazi tunatakiwa kufanya ikiwemo kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba tunaowapata Mara ya kwanza kuendelea kuwa nao,” alisema Dk. Ndugulile.

Naye Meneja Mpango wa Taifa wa Damu salama, Dk. Magdalena Lyimo amesema kuwa Mpango una mkakati wa kuboresha mfumo wa ukusanyaji taarifa na Takwimu za kielektroniki unaunganishwa nchi nzima ili kuleta tija na ubora wa huduma za damu salama nchini.

Kwa upande mwingine Dk. Magdalena amesema kuwa Mpango umefanikiwa katika kipindi cha Mwaka 2018 kwa kushirikiana na timu za Mikoa na Halmashauri ulikusanya jumla ya chupa 307,835 ambayo ni sawa na Chupa sita kwa kila watu 1000, huku Shirika la Afya Duniani linapendekeza kukusanya chupa 10 kwa kila watu 1000, makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la chupa 73,882 sawa na 32% ikilinganishwa na Takwimu za 2017.

Dk. Magdalena Lyimo aliendelea kusema kuwa kwa Mwaka 2018, wastani wa chupa 25,653 zilikusanywa kila mwezi na damu zote zilipimwa magonjwa ya HIV,Kaswende pamoja na makundi ya damu, huku matarajio ni kuongeza damu hadi kufikia chupa 375,000 kwa Mwaka 2019.

Mwisho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Dk. Biteko aagiza uboreshaji huduma za afya kwa wazee

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaTangulizi

Wanawake walalamikia ukubwa kondomu za kike, waomba zipunguzwe

Spread the loveWataalamu wa afya wilayani Ileje mkoani Songwe wameagizwa kuanza kutoa...

AfyaHabari Mchanganyiko

Madaktari wazawa watenganisha watoto mapacha walioungana

Spread the loveHospitali ya Taifa Muhimbili kwa mara nyingine imeandika historia kwa...

Afya

DC Mpanda aagiza maji ya visima yapimwe kudhibiti kipindupindu

Spread the loveMkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf ameziagiza mamlaka za...

error: Content is protected !!