April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Hosni Mubarak afariki dunia

Hosni Mubarak

Spread the love

RAIS wa zamani wa Mirsi, Hosni Mubarak (91) amefariki dunia leo tarehe 25 Februari 2020, wakati akipatiwa matibabu jijini Cairo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kifo cha Mubarak kimetangazwa leo na Televisheni ya Taifa ya Misri, ambapo imeelezwa kwamba, alifariki dunia katika Hopitali ya Jeshi.

Mtoto wake Alaa amesema, baba yake alikuwa na hali mbaya zaidi Jumamosi iliyopita, na kwamba alifikishwa hospitali na kuwa chini ya uangalizi wa madaktari tangu mwishoni mwa Januari.

Rais Mubaraka aliyeongoza nchi hiyo kwa miaka 30, aliondolewa madarakani kwa maandamano mwaka 2011, kutokana na wananchi kupinga utawala wake kwa kile walichosema kutamalaki kwa umasikini, rushwa na mateso kutoka kwa polisi wake.

Baada ya kuondolewa madarakani, alifikishwa mahakamani na mwaka 2017, alibainika kutenda jinai ya kuua watu wake waliokuwa wakiandamana kumpinga.

Hata hivyo, yapo madai kwamba Mubarak alifariki wiki kadhaa baada ya kufanyiwa upasuaji.

error: Content is protected !!