July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hoseah kuwashughulika wagombea watoa rushwa

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk.Edward Hoseah

Spread the love

MKURUGENZI wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah amejitapa mgombea yeyote atakaye toa rushwa kwa wapiga kura ili apigiwe kura atawashughulia. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).

Kauli hiyo ya Hoseah inakuja wakati kura za maoni kuwapata wagombea wa nafasi za ubunge unaofanywa na baadhi ya vyama mbalimbali huku Chama Cha Mapinduzi CCM kikionyesha kuongoza kwa kutoa rushwa katika mchakato huo.

Takukuru mara kwa mara katika kipindi cha uchaguzi kimekuwa kikitoa kauli hizo lazima huku baadhi ya wagombea wakionekana wakitoa rushwa nje nje bila kushughulikiwa na taasisi hiyo nyeti.

Dk.Hoseah amesema kipindi hiki haponi mtu kwa atakayetoa au kupokea rushwa atawashughulikia bila kujali nafasi zao na kuwaonya wananchi wasidanganywe kwa kuuza utu wao kwa kuhongwa na wagombea kwa kuwa kufanya hivyo ni kununuliwa utu wao.

“Kipindi hiki Takukuru hatuna mchezo kwa yeyote atakayetoa wala kupokea rushwa kipindi hiki hakuna biashara ya wananchi kuwaambia wagombea sasa unaniacheje ni marufuku tutawashughulia”amesema Dk.Hoseah.

Amejitapa kuwa taasisi yake imemwaga askari wake kila kona kuwashugulikia wagombea watakaokiuka sheria kwa kutoa rushwa ili wanunue uongozi na kusema wamejipanga vilivyo.

error: Content is protected !!