Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Hofu yatanda Simba kuambukizwa Corona Afrika Kusini
Kimataifa

Hofu yatanda Simba kuambukizwa Corona Afrika Kusini

Spread the love

 

SIMBA na Puma katika bustani ya wanyama ‘zoo’ nchini Afrika Kusini huenda wameambukizwa virusi vya corona kutoka kwa wahudumu wao. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Hayo yamebainishwa katika utafiti uliofanywa na wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Pretoria na kuchapishwa jana tarehe 18, 2022 katika jarida Peer Review.

Wanasayansi hao wameonya kuhusu hatari ya kirusi kipya kutokea iwapo virusi hivyo vitasambaa katika hifadhi nyingine za wanyama na kusambazwa tena kwa binadamu.

Utafiti huo ulifanywa baada ya wanyama hao kuugua na dalili ambazo zinafanana na zile za virusi vya corona kwa binadamu ikiwemo tatizo la kupumua, kutokwa na kamasi na kikohozi kikavu.

Watafiti hao walisema vipimo vilivyofanywa kwa wanyama hao vilionesha kwamba wameambukizwa corona huku data zikisema kwamba waliambukizwa ugonjwa huo na wafanyakazi waliokuwa wakiwahudumia.

Watafiti hao waliongeza kwamba wahudumu wa hifadhi hizo za wanyama walikuwa na virusi vya corona walivyosambaziana wakati huo lakini hawakuonesha dalili zozote.

Wamependekeza hatua kama vile kuvaa barakoa wakati wanapowahudumia wanyama hao. Utafiti huo umechapishwa katika jarida la virusi la Peer Review

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!