May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hofu ya corona: Kanisa ‘tusimjaribu Mungu’

Askofu Isaac Aman, wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha

Spread the love
ISAAC Aman, Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha amewataka Watanzania kutomjaribu Mungu katika kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Katika waraka wake kwa waumini aliouita ‘Kutembea Pekupeku Juu ya Mbigili,’ Askofu huyo amesema, watu wanatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari kwa maana, ugonjwa huo upo na unatesa mataifa mengi duniani.

“Tusimjaribu Mungu kwa kufanya uzembe na maisha yetu, turejee tahadhari za kuzuia maambukizi bila ya kuwa na hofu,” amesema Askofu Aman na kwamba, amesukumwa na dhamira nyema kuandika waraka huo.

“Hali inayoonekana sasa ni kwamba, mahali pengi watu wamejitangazia kwamba hakuna corona na hivyo, hakuna haja ya tahadhari.

“Maji ya kunawa kanisani yameondolewa, na pengine yapo lakini watu hawanawi tena kwa imani kwamba hakuna corona. Ile tahadhari ya kutoshikana mikono watu wamejiondolea wenyewe kwa imani kwamba, hakuna corona,” amesema.

 

Amesema, inalazimika kutengeneza utamaduni mpya huku akitahadharisha kwamba, jamii inapaswa kutafakari upya kwa kuwa mwenendo wa sasa una mashaka.

Askofu Amani amewataka mapadri na watawa kuchukua tahadhari, huku akisisitiza umuhimu wa kila mmoja kuchukua tahadhari kwa manufaa yake na wengine.

Mpaka leo tarehe 21 Januari 2021, taarifa za ugonjwa huo zinaeleza kwamba jumla ya watu 97,408,558 wameambukizwa virusi hivyo, waliofariki wamefika 2,085,827 na waliopona ni 69,970,731.

error: Content is protected !!