July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Hofu kuu Uingereza

Spread the love

HALI ya wasiwasi iliyoanzishwa na upigaji kura wa Uingereza kuondoka Jumuiya ya Ulaya (EU) imekumba chama kikubwa cha upinzani cha Leba.

Nusu ya Baraza la Mawaziri la upinzani linatarajiwa kujiuzulu hii leo likilalamikia jinsi kiongozi wao Jeremy Corbyn alivyoongoza kampeni ya kura za maoni.

Heidi Alexander, Wa kwanza kuondoka alikuwa Waziri wa Afya aliyesema kuwa Corbyn hana kipaji cha kushughulikia matatizo yanayokumba Uingereza kwa wakati huu.

Awali, Hilary Benn, Waziri wa Upinzani wa Mashauri ya Kigeni aliachishwa kazi kwa kile kilichoelezwa Corbyn alidai kuwachochea wenzake waondoke katika baraza hilo iwapo Corbyn, atakataa kuheshimu mswada wa kutokuwa na imani kwake.

Wafuasi wengi wa Leba walipiga kura kwa Uingereza kujiondoa katika Jumuiya ya Ulaya.

Tarehe 23 Juni mwaka huu Uingereza ilipiga kura ya kujiondoa EU kwa madai ya kubanwa katika mambo mengi ikiwa ni pamoja na sarafu yake kushuka, ajira kuchukuliwa na wageni.

Pia ongezeko la bidhaa kutoka nchi wanachama wa umoja huo zilizokuwa zikiingia Uingereza na kusababsha bidhaa zinazozalishwa ndani ya taifa hilo kukosa soko.

Hata hivyo, China imesema kuwa hatua ya Uingereza kuondoka kwa muungano wa Ulaya italeta msukosuko wa siku nyingi katika uchumi wa dunia.

China Lou Jiwei, Waziri wa Fedha wa China amesema, ni vigumu kutabiri matokeo lakini yanaweza kuonekana hata ndani ya kipindi cha miaka 10.

Licha ya hilo Lou amesema, masoko yameathirika kutokana na kujiondoa kwa Uingereza.

Hatua ya raia wa Uingereza kupiga kura ya kujiondoa kwenye umoja huo imeonekana kumuumiza David Cameron, Waziri Mkuu wa taifa hilo ambapo tayari ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa kushawishi raia wengi kusalia katika muunganohuo.

Chanzo BBC

error: Content is protected !!