Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Hizi hapa sheria, kanuni za habari zilizorekebishwa mwaka mmoja wa Rais Samia
Habari Mchanganyiko

Hizi hapa sheria, kanuni za habari zilizorekebishwa mwaka mmoja wa Rais Samia

Waandishi wa Habari
Spread the love

 

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imefanikiwa kurekebisha sera na kanuni zinazosimamia sekta ya habari nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Nape ameanika mafanikio hayo leo Jumatatu, tarehe 14 Machi 2022, jijini Dar es Salaam, akitaja mafanikio ya Serikali hiyo, kuanzia Machi 2021 hadi Februari mwaka huu.

Waziri huyo wa habari amesema, tarehe 12 Septemba 2021, Rais Samia aliunda wizara mpya ambayo anaiongoza kwa sasa, kufuatia kilio cha muda mrefu cha wadau wa habari, waliotaka sekta ya habari iondoke kwenye Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

“Rais Samia akiwa tu na miezi kama mitano toka aingie madarakani alifanya uamuzi wa busara na wa kizalendo kuunda wizara mpya, hii wizara haikuwepo kabla yake, imeundwa kufuatia kilio cha muda mrefu cha wadau kutaka sekta ya habari iondolewe ilipokuwa,” amesema Nape.

“Ilikuwa chini ya wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo, ikaondolewa na ikaja kuundwa na sekta ya mawasiliano iliyokuwa chini ya wizara ya ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi. Uamuzi wa sekta ziungane ni hatua kubwa ya kisera ndiyo yametufikisha hapa.”

Mbali na uundwaji wa wizara hiyo, Nape amesema sera mbalimbali zinazosimamia sekta hiyo zinapitiwa, ikiwemo Sera ya Posta ya 2003, Sera ya Utangazaji 2003, Sera ya Tehama, kwa ajili ya kuziboresha na kuzipa uwezo wa kufanya kazi.

“Sasa sera mbalimbali tunazipitia ili tuone namna ya kuziboresha zikidhi mahitaji ya wakati na mazingira tuliyonayo. Hili limefanyika kwa wakati wake, baada ya kuunda wizara,” amesema Nape.

Wakati huo huo, Nape ametaja sheria zilizofanyiwa marekebisho katika kipindi hicho, ambazo ni Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010, ambapo leseni ya biashara za simu za mkononi imeondolewa ili zisambae kwa wingi kwa wananchi wapate mawasiliano.

“Marekebisho hayo yamewapa wawekezaji wa huduma za maudhui muda wa miaka miwili kujenga miundombinu, zamani ilikuwa ukipewa leseni unapewa muda wa mwaka mmoja unatakiwa uwe umekamilisha, sisi tumeongeza ili tuwape motisha wawekezaji,” amesema Nape.

Nape ametaja amesema sheria nyingine iliyofanyiwa marekebisho ni Sheria ya Shirika la Posta ya 1993, iliyorekebishwa ili kuipa nguvu kisheria ya kufanya shughuli zake hasa za kidigitali.

Katika hatua nyingine, Nape ametaja kanuni zinazosimamia sekya ya habari na mawasiliano, zilizorekebishwa kwenye kipindi hicho, ikiwemo Kanuni ya Utangazaji kwa Njia ya Kidigitali ya 2018, ambayo imerekebishwa ili matangazo ya runinga yawafikie wananchi wengi.

Waziri wa Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye

“Mabadiliko ya kanuni hii yamewezesha chaneli za bure karibu 14 kuonekana kwenye visimbuzi vya DSTV na Zuku, kwa maana ya kuongeza wigo wa utazamaji,” amesema Nape.

Waziri huyo wa habari ametaja kanuni nyingine iliyofanyiwa marekebisho kuwa ni Kanuni za Leseni za Mawasiliano ya Kielektroniki, 2018, iliyorekebishwa ili kuongeza uwekezaji kwenye sekta ya mawasiliano ya kielektroninki.

Amesema marekebisho hayo yamegusa maeneo manne, ambayo ni kupunguza ada za baadhi ya leseni.

Nape amesema, eneo lingine ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Waziri mwenye dhamana ya mawasiliano, kushiriki kwenye mchakato wa kuuzwa kwa makampuni ya mawasiliano.

“Unajua hapa kwa kukua kwa sekta kumeanza kufanyika wakati mwingine mauziano ya kampuni ambayo ya hisa, tukadhani ni vizuri kuwe na jicho la serikali, kwenye biashara ile ya kuuziana ili maslahi ya nchi,” amesema Nape.

Nape amesema eneo lingine la marekebisho hayo, ni ufutwaji wa kifungu kinachoruhusu kampuni kubwa kufanya malipo ya ada kwa fedha za ndani, na kuwa kwa sasa kanuni hizo zinaelekeza kodi au tozo zilipwe kwa fedha za kigeni hasa Dola za Marekani.

Nape amesema, marekebisho mengine yameondoa zuio la matangazo ya kubahatisha katika vyombo vyahabari. Pia, ada ya maombi ya leseni ya maudhui ya mitandao imepunguzwa kutoka Sh. 100,000 hadi 50,000, wakati ada ya mwaka imepungua kutoka Sh. 1 milioni hadi 500,000.

Amesema, marekebisho mengine aliyafanya siku tatu zilizopita kwenye Kanuni ya Maudhui ya Mtandao ya 2020, kwa kuondoa leseni kwa watoa maudhui mbalimbali, ikiwemo maudhui, michezo na wasanii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!