Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hizi hapa sababu za Mbatia kung’olewa NCCR-Mageuzi, Msajili abariki
Habari za SiasaTangulizi

Hizi hapa sababu za Mbatia kung’olewa NCCR-Mageuzi, Msajili abariki

Joseph Selasini, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya NCCR Mageuzi
Spread the love

 

HALMASHAURI Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi, imemsimamisha Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, James Mbatia na Makamu Mwenyekiti wake Bara, Angelina Mtaigwa, kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ukiukwaji wa maadili. Anaripoti Bupe Mwakiteleko, Dar es Salaam … (endelea).

Uamuzi huo umetangazwa leo Jumamosi, tarehe 21 Mei 2022 na Mwenyekiti wa kikao cha halmashauri hiyo kilichoketi jijini Dar es Salaam, Joseph Selasini.

Akisoma maazimio ya halmashauri hiyo, Selasini amedai Mbatia amesimamishwa katika wadhifa huo kutokana na kutokuwa na mahusiano mazuri na makatibu wake.

Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Martha Chiomba, alidai kulazimishwa kujiuzulu na Mbatia, tuhuma ambazo mwanasiasa huyo alizikanusha.

“Tulielezwa jinsi ambavyo mwenyekiti alimtaka katibu mkuu ajiuzulu na ikumbukwe hana zaidi ya mwaka ndani ya chama na katika mjadala tumekubaliana alikuwa anabadilisha makatibu wakuu jinsi anavyotaka. Sasa huyu ni katibu wa sita tangu alivyokuwa mwenyekiti,” amedai Selasini.

Selasini ametaja sababu nyingine za Mbatia kusimamishwa, akidai anatuhumiwa kwa kukisabisha chama hicho kisishiriki mikutano mbalimbali iliyotitishwa kwa ajili ya kujadili masuala ya demokrasia ya vyama vingi, ikiwemo ulioitishwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).

Amedai, awali chama hicho kilikataa kushiriki vikao hivyo hadi Serikali itakapokuwa na nia njema dhidi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani, ikiwemo kuachwa huru kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, aliyekuwa rumande katika Gereza la Ukonga, kwa tuhuma za ugaidi.

Selasini amedai, baada ya Mbowe kuachwa huru Machi 2022, NCCR-Mageuzi haikuwa na kikwazo cha kushiriki vikao hivyo lakini Mbatia aliitisha kikao cha kamati cha dharura kubatilisha uamuzi huo.

Selasini amedai maazimio ya halmashauri hiyo kumsimamisha Mbatia ni halali, kwani akidi ya wajumbe wake ilikidhi matakwa ya kisheria ambapo waliohudhuria ni 52 kati ya wajumbe 82.

“Kabla ya mjadala haujaanza ulizuka mjadala wa Mwenyekiti wa chama kutokuwepo katika mkutano huu na taarifa ilitolewa kwamba anazo taarifa za mkutano akishiriki kuuitisha na baada ya kusubiri kwa muda bila kujulikana na wajumbe wako tayari ukumbi tukaona mkutano uendelee,” amesema Selasini.

Akizungumzia uamuzi huo, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, amesema utaratibu uliotumika kuchukua hatua hiyo ni halali kwa kuwa ulifuata sheria.

“Kimsingi nilikuwepo, nimeona akidi imesomwa wajumbe wapo na walijitamulisha na sisi tuna orodha yetu ya wajumbe ofisini, kwa hiyo tutaenda kulinganisha na tulio nao ofisini,” amesema Nyahoza na kuongeza:

“ Kwa jinsi akidi ya wajumbe ilivyosomwa imetimia na kama imetimia kikao ni halali na utaratibu umefuatwa kwa mujibu wa sheria wa kuwasimamisha.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!