May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hivi serikali inatambua madhara ya Zebaki?- Mbunge ahoji

Waziri Mkuu akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, inatambua madhara ya afya kwa binadamu, mimea na mazingira yanayosababishwa na matumizi ya kemikali ya Zebaki katika shughuli za uchenjuaji madini. Anaripoti Nasra Bakari, DMC…(endelea

Profesa Shukrani Manya, Naibu Waziri wa Madini ametoa maelezo hayo bungeni jijini Dodoma leo tarehe 3 Mei 2021, akijibu swali la Hawa Chakoma, (Viti Maalumu) aliyetaka kujua, kwa kiasi gani serikali inafahamu madhara yatokanayo na madini ya zebaki.

“Je, ni kwa kiasi gani serikali inafahamu madhara yatokanayo na madini ya Zebaki?” amehoji Chakoma

Profesa Manya amesema, miongoni mwa madhara ya kemikali hiyo kwa binadamu ni kuathiri mifumo ya ufahamu, uzazi, upumuaji na kusababisha magojwa mbalimbali kama magojwa ya figo, moyo na saratani.

“Aidha kemikali hiyo huweza kuathiri viumbe hai wa majini na nchi kavu pindi Zebaki inapotiririka na kuingia kwenye vyanzo vya maji.

“Njia zinazopelekea kemikali ya Zebaki kuingia mwilini ni kushika, kuvuta hewa na kula vyakula vyenye viambata vya kemikali hiyo,” amesema.

Naibu huyo amesema, pamoja na athari hizo za kiafya, matumizi ya Zebaki  katika uchenjuaji wa dhahabu yameonesha uwezo mdogo wa kutoa dhahabu ambao ni chini ya asilimia 30.

Amesema, ili kukabiliana na changamoto hiyo, serikali imekuwa ikitoa elimu kwa wachimbaji wadogo kuhusu athari za kemikali na njia salama za utumiaji ikiwa ni pamoja na usakafiaji wa mialo na utumiaji wa retorts (vigida) wakati wa uchomaji . . .   .   ) ati wa uchomaji.

error: Content is protected !!