August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hivi Angola itamkumbuka Santos?

Jose Eduardo dos Santos

Spread the love

TAARIFA za kuondoka madarakani kwa Jose Eduardo dos Santos, Rais wa Angola zimeshutua wengi ndani na nje ya taifa lake, anaandika Wolfram Mwalongo.

Swali muhimu ni kwamba, Waangola watamkumbuka Santos kutokana na staili ya uongozi wake?

Uamzi huo umefanya baadhi ya Waangaola watabasamu kutokana na msoto wa miaka 37 ya utawala wa Rais Santos anayetuhumiwa kuwa fisadi.

Uamzi huo umetangazwa na Radio ya Taifa hilo. Mrithi wa kiti chake ni Joao Lourenco, Waziri wa Ulinzi na ndiye atakayeshika hatamu ya Chama cha MPLA ambacho kimekuwa madarakani tangu taifa hilo lipate uhuru mwaka 1975.

MPLA ndio chama pekee cha nchi hiyo kilichoshirikiana na Jeshi la Cuba kumwondoa mkaburu na mwaka 1979 na kumpata mwenyekiti wake mpya Rais Santos.

Ingawa hana mpango wa kurejea Ikulu mwakani, bado kiongozi huyo anateswa na kashfa za ufisadi jambo ambalo limeendelea kushusha hadhi yake hata pale atakapong’atuka.

Kwa mjibu wa mtando wa Forbes, Rais Santos anatajwa kuwa rais namba moja tajiri Afrika akifuatiwa na Mohammed VI, Mfalme wa Morocco.

Utajiri wake unakadiriwa kuwa Dola za Marekani 20 bilioni na binti yake Isabel dos Santos akiwa na utajiri wa Dola za Marekani 3.8 bilioni.

Mwanaye huyo anatajwa kuingia kwenye rekodi za wanawake matajiri Afrika huku akiendelea kufukuzia rekodi ya dunia ya wanawake matajiri wenye asili ya Afrika.

Mbali na kwamba, Angola ni miongoni mwa mataifa ya Afrika yenye hazina kubwa ya mafuta, gesi na almasi bado wananchi wake wameendelea kusota kwenye maisha ya ufukara ambapo asilimi 70 ya raia hutumia chini ya dola moja kwa siku.

Santos mwenye umri wa miaka 74 ameongoza taifa hilo kwa miaka 37 sasa, akiwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walio madarakani kwa muda mrefu, amekuwa akichuana na mwenzake Teodoro Obiang Nguema, Rais wa Guinea mwenye miaka kama hiyo (37) Ikulu.

Santos mwaka 1979 alishika hatamu ya kuongoza Angola akiwa kijana wa maiaka 34 na kutumbukia kwenye rekodi za viongozi wa Afrika walioshika madaraka hayo makubwa katika umri mdogo.

Kiongozi wa kwanza aliyeshika madaraka akiwa mdogo Afrika ni Mfalme Mswati wa III wa Swaziland 1986 akiwa na umri wa miaka 18 baada ya kurithi nafasi ya baba yake Mfalme Sobhuza II.

Mwingine ni Joseph Kabila, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) aliyeshika madaraka akiwa na umri wa miaka 29 baada ya baba yake Laurent Kabila kuuawa mwaka 2001.

error: Content is protected !!