January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hisabati, Kingereza yapatiwa mbinu mpya

Wanafunzi wa chuo wakisoma kupitia mtandao

Spread the love

SHIRIKA lisilo la kiserikali la North Mara Trust Fund linatarajia kuanzisha mradi wa kuenua (kuendeleza) elimu kwa njia ya kisasa (digital) ili kuongeza ufahamu katika masomo ya Kiengereza na Hisabati. Anaandika Faki Sosi, DSJ … (endelea).

Hatua hii inaelezwa ni kutokana na kuanguka kwa elimu nchini. Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Meneja Mradi huo, John Waigama wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Waigama amesema kuwa, Tanzania inakabiliwa na changamoto ya elimu hususani katika masomo hayo.

Ameeleza kuwa, miongoni mwa changamoto kubwa inayowakabili wananfunzi ni kutopenda na pia kutoelewa masomo hayo hivyo kusababisha kufeli.

Hata hivyo amesema, sehemu ya pili ya changamoto hiyo ni kutokana ni uhaba wa zana za kufundishia na kutumika kwa mbinu zilizopitwa na wakati.

Hivyo, mbinu hiyo mpya itasaidia kuongeza hamasa na uelewa wa wanafunzi hao. Katika kufanikisha mradi huo, wadau muhimu ni pamoja na Microsoft, Acee na North Mara.

“Tumewasiliana na wenzetu kutoka Uganda ambao wao wameshaanza huu mfumo huo kwa miaka minne sasa.

“Wameweza kupata matokeo mazuri ya kupanda kwa elimu yao kwa kiwango kizuri, nasi tumeenda kujifunza huko na tupo na mtaalamu kutoka Uganda,” amesema Waigima.

Mtaalamu wa masuala hayo kutoka Uganda, Charles Muhindo ameeleza kuwa, Uganda wamethubutu kutumia mfumo huo katika kufundisha wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari na Elimu ya Juu na kwamba; “wanafunzi wanafanya vizuri katika kufaulu masomo hayo ya hisabati na kiengereza.”

Muhindo ameleza kuwa, mtandao wa www.brainshare.or.tz ndio utakaokuwa na taarifa zote kuhusu mada mbalimbali za masomo hayo.

Na kwamba, wanafunzi watajifunza masomo hayo ambayo yamefanyiwa usanifu wa hali ya juu ili kumwewezesha kufaulu na kuongeza kuwa, wanafunzi wanaweza kusoma bila kuwepo kwa mtandao.

Aidha amesema, kupitia Runinga, Radio, DVD na vyombo vengine vya habari, kutamuwezesha mwanafunzi kufanya mtihani na kujibu maswali mbalimbali kisha kusahihishwa na baadaye kuendelea kusoma mada nyengine.

error: Content is protected !!