October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hiki ni kiburi au dharau Chadema kwa waandishi wa habari?

Spread the love

WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikiwakumbatia waandishi wa habari, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani kinawapuuza. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea).

Jana Jumatatu tarehe 13 Julai 2020, majimbo saba kati ya 10 yaliyopo jijini Dar es Salaam, yalikuwa kwenye mchakato wa kupata wagombea ngazi ya ubunge kwa kufanya kura za maoni.

Waandishi wa vyombo vya habari mbalimbali, walijitokeza kufanya kazi ya habari katika chaguzi hizo kama ilivyokuwa kwenye chaguzi za vyama vingine.

Kwenye Jimbo la Segerea, uchaguzi ulifanyika katika Ukumbi wa Baracuda, Tabata ambapo waandishi walifika eneo la mkutano huo kuanzia saa 6 mchama.

Kwenye mkutano huo, hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akitoa mongozo kwa watu waliofika eneo hilo. Mara kadhaa waandishi waliuliza utaratibu na kutaka kuingia kwenye baadhi ya matukio, hawakupata ufafanuzi.

Kutokana na kutokuwa na mwongozo wowote, ilipofika saa 12:30 jioni wakati wa maandalizi ya kutangaza motokeo ya kura za wajumbe wa ambao matokeo ya kura, waandishi waliingia ndani ili kushuhudia tukio hilo.

Soma zaidi hapa

Wahariri Tanzania wataka uwazi wa Ccm uhamie NEC, Mahakama na Bunge

Hemed Ally, Katibu wa Kanda ya Pwani alizuia waandishi kuendelea na kazi ya kuchukua picha wakati wa kutangaza matokeo.

Katibu huyo aliwaambia waandishi “tunaomba muende nje kwa kuwa kuna mambo yote tunataka kufanya.” Waandishi walitii agizo hilo.

Lakini dakika tano baadaye, Ally alisikika akitangaza mtokeo hayo huku waandishi wakiwa nje, mlangoni kukiwa na mlinzi. Tukio hilo muhimu, waandishi hawakulipata.

Pamoja na hivyo, waandishi walimtuma mjumbe mmoja wa mkutano huo kumwita Ally kwa ajili ya kufanya naye mahojiano ikiwa ni pamoja na kuwapa matokeo.

Soma zaidi hapa

Agnesta awaongoza wanaume Segerea

Ujumbe huo ulimfikia lakini hakuitikia wito, aliyetumwa alirejea kutoa majibu kwamba amefikisha ujumbe, hata hivyo kwa kuwa mlango ulikuwa wa kioo, waandishi walishuhudia akifikishiwa ujumbe huo.

Ally aliendelea kupiga stori, ilipofika saa 2 kasoro usiku, waandishi walilazimika kuondoka eneo la ukumbi huo huku wakijiuliza ‘hiki ni kiburi au dharau?

Hii ni tofauti na kile ambacho kimefanyika kwa CCM kwenye mikutano yake miwili iliyorushwa moja kwa moja na vyombo mbalimbali vya habari.

Jana Jumatatu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akizungumza jijini Dodoma, alitoa wito kwa mikutano yote ya kura za maoni, kuhakikisha inakuwa wazi na waandishi waruhusiwe kuingia.

error: Content is protected !!