Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Hiki ndio kilio cha mmiliki wa Coco Beach
Habari Mchanganyiko

Hiki ndio kilio cha mmiliki wa Coco Beach

Spread the love

ALPHONCE Buhatwa, mmiliki wa Hoteli ya Coco Beach iliyopo kwenye fukwe ya Oysterbay, jijini Dar es Salaam iliyoungua moto tarehe 22 Septemba 2019, yupo njiapanda. Anaripoti Hamis Mguta… (endelea).

Namna moto huo ulivyoanza, Alphonce anasema, haridhishwi na maelezo ya awali. Moto huo ulianza majira ya 8 mchana ambapo mmiliki wa hoteli hiyo hakuwepo eneo la tukio. Lakini mgogoro wake na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ndio unaomuumiza zaidi.

Tarehe 18 Septemba 2019 ikiwa ni siku tatu kabla ya tukio hilo kutokea MwanaHalisi ilifika katika eneo la fukwe hiyo kuzungumza na wafanyabiashara wa fukwe hiyo wakiwemo wa Coco Mihogo kuhusu agizo la serikali la wafanyabiashara hao kupisha mradi wa kimakakati unaofanyika katika fukwe hiyo na kilikutana na Buhatwa ambaye alisema kuwa kuwa hajui muafaka wake.

“Nina mashaka kama walivyokuwa na mashaka binadamu wengine, hapa nataka kufanyiwa kitu ambacho hakipo sawa na sio cha kawaida, pamoja na jambo hilo lipo mahakamani na vibali ninavyo lakini kuna watu wanataka kufanya vitu vya tofauti,” alisema na kuongeza;

“Kati yangu na Manispaa ya Kinondoni bado hatujafikia muafaka. Nimewekeza hapa (Coco Beach) pesa nyingi lakini bado sijaambiwa chochote kuhusu mradi ninaousikia.”

Amesema, awali kulikuwepo na mgogoro kati yake na serikali kupitia Manispaa ya Kinondoni ambao ulitokana na mfanyabiashara mmoja nchini kulitaka eneo hilo.

Mpaka sasa Buhatwa anasema, hajui muafaka wake baada ya kuwepo kwa mkakati wa ujenzi mpya kwenye fukwe hiyo licha ya kuwa, tayari amewekeza kiasi kikubwa cha pesa. 

“Nimepeleka malalamiko yangu kwa viongozi mbalimbali na mpaka sasa sijapata taarifa yoyote, lakini nasikia wafanyabiashara wa Coco Mihogo wamepewa notisi ya mwezi mmoja na nusu kuupisha mradi. Mpaka sasa sijapewa taarifa yoyote ila nipo radhi kupisha mradi huo endapo kutakuwa na makubaliano.

Baada ya jitihada ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji za kuuzima moto huo kutofua dafu, Buhatwa amesema kuwa ni kiasi kidogo cha mali zilizookolewa ambapo zaidi ya asilimia 80 ya mali zote katika hoteli hiyo, zimeteketea.

“Siwezi kusema thamani ya mali, ni jambo linalofanyiwa uchunguzi lakini ukumbi huwa ninaukodi Sh 1.4 milioni kwa siku,” amesema.

Buhatwa ambaye ndiye muwekezaji wa kwanza na muanzilishi wa jina la Coco Beach, alianza kufanya biashara katika eneo hilo mwaka 1994 kwa kuanza kuweka huduma ya choo.

Baadaye alianza kufanya biashara ya vinywaji ambapo mpaka eneo hilo linateketea kwa moto, alikuwa amepangisha wafanyabiashara mbalimbali ikiwemo maduka ya bidhaa za nguo, vinyago, vyakula, kukodisha ukumbi na vinywaji.

Kufuatia moto huo, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Musa Taibu amesema bado chanzo cha moto huo hakijafahamika.

“Nilipigiwa simu majira ya mchana nikiwa Mbezi Beach kikazi, nikaambiwa ukumbi wa Coco Beach unaungua moto, nikamjulisha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kinondoni ili akimbizane na askari eneo la tukio, hilo limefanyika na Fire walijulishwa kufika eneo la tukio lakini ilishindikana kwasababu moto ulizima baada ya jengo lote kuteketea.

“Chanzo cha moto bado hatujakibaini, lakini kwasababu tupo na tunachunguza tutabaini chanzo, tumeshaanza kufanya uchunguzi, tunampa pole kwa hili lililomkuta” amesema.

Katika ukumbi huo, kwa upande wa chini kuna ukumbi mwengine unaotumika kwa huduma za Kanisa la Dar es Salaam Christian Fellowship, ambao hukutana kwa ajili ya kufanya sala kila Jumapili.

MwanaHALISI Online ilishuhudia waumini wakiwamo raia wa kigeni, wakiokoa vifaa vya muziki na meza kutoka ndani ya ukumbi.

Wakati tukio la kuokoa vitu likiendelea na vilio kwa waliopoteza mali zao na ajira vikizizima, umati wa vijana uliendelea kulitumia tukio hilo wakibeba vitu mbalimbali ikiwemo Televisheni, Radio.

Tarehe 17 Septemba 2019 Benjamin Sitta ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, alitoa taarifa ya halmashauri yake kutoa notisi kwa wanaojishughulisha na shughuli fukwe hapo kupisha ujenzi wa Mradi wa Kimkakati wa kuendeleza fukwe hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

Habari Mchanganyiko

NMB yafuturisha Dar, Majaliwa azitaka Serikali za Mitaa, Taasisi zijifunze kwao

Spread the loveBENKI ya NMB imewafuturisha wateja wake walio kwenye Mfungo wa...

error: Content is protected !!