November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hiki hapa kilichomuua Mashaka wa ‘Kaole’

Spread the love

RAMADHANI Mrisho Ditopile, msanii wa maigizo katika Kundi la ‘Kaole Sanaa Group’ amefariki dunia asubuhi ya leo tarehe 20 Oktoba 2018 katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa hiyo imethibitishwa na mtoto wa marehemu Ditopile ambaye katika tasnia ya sanaa alifahamika kwa jina la Mashaka, Abdallah Ditopile akisema kuwa baba yake alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu ‘Presha’.

Abdallah ameeleza kuwa, marehemu baba yake alizidiwa hafla jana na kukimbizwa katika hopsitali ya Amana na kuwekea mashine ya kumsaidia kupumua ‘Mashine ya Oksijeni’ kutokana na hali yake kiafya kuwa mbaya.

Amesema kabla ya umauti kumfika baba yake, hospitali ya Amana alitoa rufaa ya kumpeleka Hospitali ya Muhimbili tawi la Mloganzila na kwamba wakati wakifuata taratibu za uhamisho huo, baba yake alikata roho.

Ditopile amesema kwa sasa taratibu za msiba zinapangwa kwa kaka mkubwa wa marehemu maeneo ya Ilala Sokoni, na kwamba taarifa za mahali ambako msiba utakuwepo na siku ya mazishi zitatolewa baadae baada ya wanandugu kuamua.

error: Content is protected !!