Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Hii ni haki yake Lissu’
Habari za Siasa

‘Hii ni haki yake Lissu’

Tundu Lissu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki
Spread the love

OMBI la aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chaadema), Tundu Lissu kwamba serikali imlinde, limetiliwa mkazo na chama chake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). 

Chadema kimeeleza, kitisho cha kung’oa uhai wa Lissu kinapaswa kuiamsha serikali tena na kumuhakikishia usalama kwa kuwa ‘ni wa jibu wake (serikali) kikatiba.’

“Serikali inawajibika kumlinda Lissu, ni wajibu wake kikatiba” amesema John Mrema, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Itikadi na Uenezi ya chama hicho alipoongea na chombo kimoja cha habari nchini.

Amesema, Lissu ambaye alikuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ametaja kwa jina mtu anayejigamba kutaka kumshughulikiwa na kwamba mamlaka zinamjua hivyo ni wajibu kwa serikali kuchunguza na kuchukua hatua.

Lissu ambaye anaishi nchini Ubelgiji, tangu aliposhambuliwa kwa risasi nyumbani kwake, ‘Area D’ mjini Dodoma tarehe 7 Septemba 2019, amesisitiza kuwa hatarejea nchini hadi atakapohakikishiwa usalama wa maisha yake.

“Nimebadili msimamo wangu wa kurejea Tanzania mwishoni mwa mwaka huu. Hii ni kwa sababu, bado naamini kuwa mazingira ya kiusalama kwangu, bado sio mazuri. Kuna watu kule nchini, wanaendelea kutoa vitisho kuwa wataangamiza maisha yangu.

“…kuna mtu anaitwa Musiba. Ametangaza mitandaoni na kusema hadharani, kwamba Lissu atapigwa risasi siku akitua tu nchini,” alisema Lissu alipokuwa katika mahojiano yake na kituo televisheni cha Sauti ya Marekani (VOA).

“Sisi kama chama, tunaunga mkono kauli yake kwamba kwa sasa tunataka athibitishiwe usalama wake pindi atakaporudi, na wenye mamlaka ya kuhakikisha usalama wake ni Serikali,” amesema Mrema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!