Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Hii hapa ahadi ya ACT-Wazalendo kwa Watanzania
Habari za Siasa

Hii hapa ahadi ya ACT-Wazalendo kwa Watanzania

Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu
Spread the love

 

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimesema ndoto yake kuu si kushika dola bali kuwakomboa wananchi kiuchumi na kijamii. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 18 Februari 2023 na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, katika uzinduzi wa ahadi ya chama hicho kwa Watanzania, jijini Dar es Salaam.

“Chama cha siasa ni zaidi ya kusanyiko la watu, chama cha siasa lazima kiwe na malengo, chama cha siasa ni zaidi ya kushika dola. Malengo ya chama makini ni kuukomboa umma, kufanyia kazi changamoto za umma. Nafasi za kimadaraka ni nyenzo tu ya kutekeleza malengo ya chama cha siasa,” amesema Shaibu.

Amesema kuwa, ili ACT-Wazalendo itekeleze malengo hayo kinapaswa kujipanga kazi ambayo kimeanza kuifanya tangu kuanzishwa kwake Mei 2014.

“Sio kazi ndogo, sisi tumekusudia ili tuweze kutekeleza wajibu huo ipasavyo lazima tujenge taasisi imara ambayo inakubalika katika jamii ya watanzania,” amesema Shaibu.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!