August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

HESLB yatoa saa 48 kwa wadaiwa sugu

Spread the love

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu nchini (HESLB), imetoa siku mbili kuanzia leo Ijumaa ya 29 Julai kwa wadaiwa sugu kujisalimisha wenyewe kabla ya kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yao, anaandika Faki Sosi.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam, Jerry Sabi Kaimu mkurugenzi mkuu wa HESLB amesema kuwa bodi hiyo italazimika kufungua ofisi zake katika siku za Jumamosi na Jumapili wiki hii ili kuwapa nafasi wadaiwa sugu kufika na kujieleza.

“Tarehe 30 na 31 Julai mwaka huu, ofisi zetu zitakuwa wazi na hii itakuwa fursa kwa wadaiwa wote kufika ili tuwasikilize na kuwapa taarifa za madeni yao,” amesema.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya HESLB, wadaiwa ambao hawatajisalimisha na kuanza kulipa madeni yao watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwapeleka mahakamani, kuwatoza faini, kuwazuia kusafiri nje ya nchi, na kuwanyima fursa ya kusoma nje ya nchi.

error: Content is protected !!