July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

HESLB watoa maelekezo kwa wasiopata mikopo

Spread the love

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imetoa utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya wanafunzi ili kuondoa usumbufu wakati wa masomo, anaandika Faki Sosi.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Omega Ngole, Ofisa wa Elimu na Uhusiano wa HESLB, amesema kuwa mwanafunzi mwenye malalamiko anapaswa kuwasiliana na Ofisa anayesimamia dawati la mikopo.

Amesema kuwa ofisa huyo anakuwepo kwenye vyuo mbalimbali na kwamba anashughulikia masuala hayo kwa ukaribu.

“Ofisa kwa kushirikiana na uongozi wa chuo husika watapata majibu ya malalamiko yao, na ikiwa hajapata majibu basi uongozi wa chuo utawasiliana na Ofisi za kanda za HESLB, na kwa watapata majibu ndani ya siku mbili,” amesema Ngole.

Amewataka maofisa wanaosimamia mikopo kuhakikisha kuwa taarifa zote muhimu zinafika kwa wakati kwa ajili ya kuandaa malipo ya wanafunzi.

Ngole amesema kwa mujibu wa sheria ya vigezo vya kupata mikopo ya elimu ya mhusika anapaswa awe raia wa Tanzania, aombe kupitia mtandao wa bodi, awe amechaguliwa kujiunga na chuo kupitia NACTE au TCU kama mwanafunzi wa muda wote.

Ameongeza kuwa sifa za kupata mkopo kuwa awe mwanafunzi anayeendelea na masomo na amefaulu mitihani, asiwe mnufaika wa mkopo au ruzuku kutoka taasisi nyingine au watu wengine aliyemaliza kidato cha sita mafunzi ya ufundi.

error: Content is protected !!