July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Heshima za mwisho zatolewa kwa Dk. Makaidi

Spread the love

VIONGOZI mbalimbali wametoa salamu za rambirambi kwenye shughuli za mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Dk. Emmanel Makaidi katika viwanja vya Kareem Jee leo Jijini Dar es Salaam, Anaandiak Faki Sosi …(endelea).

Salamu hizo zilitolewa na wanasiasa, viongozi wa serikali, ndugu, jamaa na marafiki kwa wanafamilia ya Dk. Makaidi.

Msajiri wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungu amewataka Watanzania kutohusisha kifo cha Dk, Makaidi na masuala ya siasa na kuwata Watanzania kumuenzi kiongozi huyo kwa kuitunza amani ya nchi kwa kushiriki katika uchaguzi mkuu kwa kuitunza amani.

“Marehemu amewahi kuwa mwanasiasa ambaye ameshiriki katikati haraka mbalimbali za kisiasa licha ya kuwa muasisi wa chama cha NLD, pia alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa baraza la vyama vya siasa nchini mwaka 2002,” amesema Mutungi.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu amesema kuwa, Dk. Makaidi alikuwa ni miongoni mwa wapambanaji katika kuleta mabadiliko ya nchi.

“Nilimfahamu Dk. Makaidi tangu mwaka 1990 na alikuwa mpambanaji wa kweli katika harakati za mabadiliko, kifo chake hakitaturudisha nyuma, tutaendelea katika mapambano haya ambapo kuna ishara ya ushindi,” amesema Baregu.

Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia amesema kuwa kiongozi huyo ambaye ni mwanamabadiliko alipanda jahazi hilo la mabadiliko kutokana na utashi wake wa kisiasa wa kutaka maslahi ya wananchi yawe mbele.

“Tulipo kuwa bungeni katika kutetea katiba ya wananchi marehemu aliwahi kukataa kuchukua posho kwa ajili ya kutetea katiba ya wananchi wa taifa hili na tulimsikiliza kwa kila asemacho kutokana na busara na elimu yake,” amesema Mbatia.

Muwakilishi wa Klabu ya Soka ya Simba, Daniel Kamuna ambaye amesema kuwa klabu hiyo inasikitika kumpoteza Dk. Makaidi kutokana mchango mkubwa aliotoa katika kuhakikisha Simba inafanya vizuri.

“Miaka ya 80 Klabu ya Simba ilipofungwa mfulilizo na Yanga tukamchagua kuwa mwenyekitu wa klabu yetu, mabadiliko yalitokea kwa kuwafunga Yanga,’’ amesema.

Mwakilishi wa NLD, Hamisi Mfaume akitoa pole kwa familia amesema kuwa chama hicho kimepata pigo kubwa kwa kumpoteza mwenyekiti wake ambaye alipambana kwa ajili ya kufanya chama hicho kidogo kupata nguvu.

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Peter Mzirai amesama kuwa mwenyekiti muasisi wa baraza hilo, Dk Makaidi ametoa mchango mkubwa katika tasnia ya siasa pia changamoto kubwa kwa wanasiasa wengine.

Dk. Makaidi amefariki dunia Oktoba 15 mwaka huu kwa ugonjwa wa shinikizo la la damu (BP).

error: Content is protected !!