December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

HELSB  yakumbushia madeni

Spread the love

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini imewataka wanafunzi walionufaika na mikopo kupitia bodi hiyo waliohitimu na wanaohitimu kulipa madeni yao kwa wakati ili kuwezesha wanafunzi wengine wanavigezo kukopeshwa. Anaandika Regina Mkonde.. (endelea).

Kwa mujibu wa Sheria Na. 9 ya Bodi ya Mikopo inasema kuwa mwanafunzi wa elimu ya juu anayekidhi vigezo hupewa mkopo wa elimu kwa ajili ya gharama za chakula na malazi, vitabu na  mahitaji maalum ya vitivo, gharama za mafunzo kwa vitendo na utafiti pamoja na ada ya masomo.

Kwa mwaka wa fedha wa 2015-2016 bodi imetoa mikopo kwa wanafunzi 122,486 sawa na kiasi cha shilingi bilioni 459, kati ya wanafunzi hao, wanafunzi wa mwaka wa kwanza 53,618 wamepata mikopo pia wanafunzi 4,453 ni yatima, 1397 wenye ulemavu. Wanafunzi wa kiume 85,827 na wa kike 36,659.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo jijini Dar Es Salaam Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi, Omega Ngole, amesema kuwa kwa mwaka wa fedha wa 2015-2016 idadi ya wanafunzi waliopata mikopo imeongezeka.

“Kwa mwaka wa fedha wa 2015-2016 idadi ya wanafunzi waliopata mikopo imeongezeka ukilinganisha na mwaka 2014-2015, hii yote ni matokeo ya jitihada nzuri za ukusanyaji madeni kutoka kwa walionufaika na mikopo ya elimu ya juu. Mwaka wa fedha wa 2014-2015 bodi ya mikopo ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 21.7,kwa kipindi cha miezi 6 iliyopita julai hadi disemba mwaka jana zilikusanywa bilioni 12.1.”Alisema Ngole

Ngole alibainisha vipaumbele vya kozi ambazo wanafunzi wanasoma walipata mikopo wa kwanza ukilinganisha na kozi nyingine ikiwa pamoja na kozi ya udaktari wa binadamu, meno, uuguzi na ualimu wa hisabati na sayansi.

Wanafunzi ambao wana vigezo ila wamekosa mikopo wametakiwa kukata rufaa, kama watakuwa wamekidhi vigezo vya bodi watapewa mikopo, bodi imekanusha kauli ya baadhi ya wanafunzi kukosa mikopo kutokana na ukosefu wa fedha bali bodi imedai kuwa wanafunzi wasiokidhi vigezo ndiyo wasiopata mikopo pia wapo wanafunzi wengine ambao hawataki mikopo

“Mikopo hutolewa kwa kuzingatia miongozo ya bodi,ukiona mwanafunzi hajapata mkopo kwa mwaka huu ujue hajakidhi vigezo ama hana sifa,bodi inachambua wanafunzi wenye sifa watakao pewa mikopo,kwa mtui asiyeridhika na uamuzi wa bodi anatakiwa kukataa rufaa kupitia mtandao wa bodi.”Alisema Ngole

Bodi ya Mikopo imewataka waajiri na waajiriwa kutoa taarifa za waajirwa wapya siku 30 baada ya kuanza kazi, pia kila katikati ya mwezi yaani siku ya 15 waajiri wanalazimika kupeleka makato ya deni la kila mwajiriwa anayedaiwa na bodi.

“Waajiri kutoka taasisi na kampuni za serikali na zisizo za kiserili kupeleka majina ya waajiriwa wao wote kwenye bodi ili bodi ichambue wanaodaiwa,na walionufaika na mikopo ambao wamejiajiri ama kuajiriwa nje ya nchi wanatakiwa kutoa taarifa ya maeneo walipo na anuani zao pia kulipa kiai cha fedha kilichopangwa na bodi.”Aliongeza Ngole

Kwa wasiolipa kodi ndani ya miezi 12 tangu kuhitimu masomo yao watatozwa faini ya asilimia 10 kwa kila wasilisho wasilowasilisha na muajiri asipopeleka makato ya muajiriwa wake atatozwa faini ya kiasi cha shilingi milioni 7.

error: Content is protected !!