July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hekta 500 za misitu Mvomero zateketezwa

Sehemu ya Msitu wa Asili wa Mkingu, uliopo wilayani ya Mvomero

Spread the love

HEKTA 515 za Msitu wa Asili wa Mkingu na ule wa Hifadhi Kanga uliopo wilayani Mvomero, Morogoro imeharibiwa vibaya baada ya wananchi kuvamia na kufanya shughuli za kilimo. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).

Hayo yalibainishwa na Meneja mradi wa kuongeza thamani ya misitu ya Tao  la Mashariki (AVA), Hassan Chikila  Wilaya ya Mvomero alipokuwa akizungumzia changamoto zinazoukabili mrad huo.

Chikila alisema mradi huo wa miaka mitano ulioanza mwaka 2013 lengo lake ni kuchangia jitihada za usimamizi wa misitu unatekelezwa kwa ubia kati ya Shirika la Kuhifadhi Misitu Asilia Tanzania (Tfcg), Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu (MJUMITA), Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) na Halmashauri ya Mvomero unafadhiliwa  na Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).

Amesema, kwa mujibu wa tafiti walizofanya walibaini uharibifu huo na kwamba, msitu wa asili wa Mkingu hekta 475 ziliharibiwa huku katika msitu wa hifadhi wa Kanga hekta zilizoharibiwa ni 40.

“Mradi huo utahusisha vijiji 31 vya Mvomero, kwa sasa utekelezaji umeanza katika vijiji sita ambavyo ni Difinga, Bwage, Msolokelo, Mziha, Masimba na Makuyu,” Amesema.

Amefafanua kuwa, Kijiji cha Difinga ndicho kilicho na changamoto kubwa kwa kuwa, wananchi 39 wanajishughulisha na kilimo ndani ya misitu wa Mkingu wakiongozwa.

Katika jambo la kushangaza, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Adam Hussein anashiriki kilimo katika msitu huo huku wakazi wa Kijiji cha Msolokelo wakilima kandokando ya misitu pamoja na kukata miti kwa ajili ya kuchoma mkaa.

Hata hivyo, Hussein alikiri kufanya kilimo ndani ya msitu huo na kuahidi kuacha baada ya kupata mafunzo kupitia mradi na kwamba, atawaelimisha wananchi wengine.

Akizungumzia changamoto Chikila amesema, baadhi ya vijiji vimetenga maeneo machache kwa ajili ya misitu, uvamizi wa misitu ya serikali kwa kigezo cha kutofahamu mipaka.

Kwa upande wa mafanikio amesema, “tumewatafutia wananchi hao njia mbadala za kujitafutia kipato ili kuepukana na uharibifu wa misitu lakini pia kuhamasisha katika kujiunga na vikundi vya hisa na Vicoba ambapo tumewezesha vikundi 108 lengo ikiwa ni kujiwekea fedha na kukopeshana.”

Amesema, wamehamasisha watalaamu kutoka Chuo Cha Kilimo cha Sokoine (SUA), kuwapatia mafunzo ili kufanya kilimo chenye tija.

Katika hatua ya kukabiliana na ukataji misitu amesema, wanakijiji 26 wametengenezewa majiko banifu kuepuka ukataji miti kiholela katika Kijiji cha Msokolokelo ikiwa ni hatua ya kutekeleza malengo ya mradi.

error: Content is protected !!