Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hekima za Ndugai kuokoa wabunge nane wa CUF
Habari za SiasaTangulizi

Hekima za Ndugai kuokoa wabunge nane wa CUF

Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa
Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa bado anaitafakari barua ambayo ameipokea kutoka kwa, Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye anatambulika na msajili wa vyama vya siasa, anaandika Hellen Sisya.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mapema leo hii, Ndugai amethibitisha kupokea barua kutoka kwa Lipumba kumtaarifu kuhusiana na uamuzi wa Baraza kuu la chama hicho wa kuwafukuza uanachama baadhi ya wabunge na madiwani kutokana na makosa kadhaa ya kinidhamu.

Ndugai amesisitiza kuwa suala la kuwaondoa uanachama ni la utashi wa vyama husika na kila chama kina utaratibu wake, hivyo bado anaitafakari hiyo barua na maamuzi yake kwa wabunge waliofukuzwa uanachama atautoa baadae.

Wabunge waliotajwa kufukuzwa uanachama ni pamoja na Severina Silvanus Mwijage, Saumu Sakala, Salma Mwassa, Riziki Ngwali, Raisa Abdallah Mussa, Miza Bakari Haji, Hadija Ally Al-Qassmy, Halima Ali Mohamed.

Mgogoro ndani ya Chama cha CUF ulianza wakati ambapo Lipumba alipoamua kujiuzulu nafasi ya uenyekiti aliyokuwa nayo na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida baada ya Chama hicho kikishirikiana na vyama vingine vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kumteua Edward Ngoyai Lowasa, waziri mkuu mstaafu kuwa mgombea wao wa nafasi ya urais kwa mwaka 2015.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

Habari za Siasa

Babu Owino: Vijana msibaki nyuma

Spread the loveMbunge wa Embakasi Mashariki nchini Kenya, Paul Ongili Owino maarafu...

error: Content is protected !!