HEKARI za misitu zaidi ya 2.8 Milioni ziko hatarini kupotea ifikapo mwaka 2030, kutokana na ongezeko la matumizi ya nishati mbadala. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Hayo amesema Dk. Medard Kalemani, Waziri wa Nishati wakati akihutubia katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa uzalishaji umeme katika mto Rufiji ‘Stigler’s Gorge, leo tarehe 26 Julai 2019.
Dk. Medard amesema hekta za misitu laki 8 hukatwa kila mwaka kwa ajili ya matumizi ya nishati mbadala. Ambapo asilimia 71.2 ya Watanzania wanatumia mkaa na kuni huku Jiji la Dar es Salaam likiongoza kwa matumizi hayo, kwa kutumia magunia laki 5 kwa mwezi.
“Kila mwaka hekta laki 8 hukatwa kwa ajili ya matumizi ya nishati mbadala, tukiendelee mwaka 2030 hekari 2.8 milioni zitakatwa kwa sababu ya nishati jadidifu.
Kwa Dar es Salaam pekee, magunia laki 5 hupelekwa na kutumika kila mwezi, watanzania asilimia 71.2 wanatumia nishati mbadala ya kuni na mkaa,” amesema Dk. Kalemani.
Dk. Kalemani amesema mradi wa umeme wa Stiglier’s Gorge utasaidia kupunguza athari za uharibifu wa mazingira, ikiwemo kupungua matumizi ya nishati ya kuni na mkaa, na kutokomeza changamoto za ukataji wa misitu.
Leave a comment