October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hekaheka yaibuka ndani ya ndege Marekani

Spread the love

HEKAHEKA imeibuka ndani ya ndege ya Jet Blue, ambapo abiriwa waliokuwa wakitoka katika uwanja wa Ndege wa San Juan (Carolina) kwenda Miami, waligoma kusafiri. Unaripoti mtandao wa habari wa CBS … (endelea).  

Abiria hao, waliuvaa utawala wa shirika la ndege hiyo wakitaka utaratibu wa umbali wa zaidi wa mita moja utumike kutoka abiria mmoja kwenda abiria mwingine ndani ya ndege hiyo ikiwa ni hatua ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.

Idadi kubwa ya abiria walioingia kwende ndege hiyo, iliwashtua abiria wenyenye na kuanza kuhoji,  iweje utawala wa ndege hiyo upuuze utaratibu wa umbali hasa katika kipindi hiki ambacho Marekani imerekodi vifo vingi vya corona kuliko mataifa yote dunani.

Abiria 145 walikuwa wamepewa tiketi ya kusafiri na ndege hiyo na kusababisha msongamano uliowashtua abiria wenyewe.

Abiria hao waliutaka utawala wa ndege hiyo kurejesha fedha kwa baadhi ya abiria kutokana na msongamano huo.

Uongozi wa Jet Blue umejitetea, kwamba kabla ya abiria hao kuingia katika ndege, ulichukua hatua ikiwa ni pamoja na viti vyake 27 vya ndege kuviondoa ili kuhakikisha kunakuwepo na umbali wa kutosha kati ya abiria na abiria.

“Kuna hofu hapa kutokana na idadi kubwa ya watu,” abiria mmoja alisema na kuongeza “kumekuwa na watu wengi zaidi ya inavyotakiwa.”

 “Hivi watu wanaweza kutekeleza agizo la kuwa na umbali wa zaidi ya mita moja ndani ya ndege?” amehoji Robin Hayes, Mtendaji Mkuu wa Jet Blue alipozungumza na kituo cha habari cha CBS na kuongeza:

“Ndio maana tukaomba kila abiria avae barakoa, kwa sababu kama ujuavyo, unapokuwa kwenye ndege hata utakapoiondoa siti ya katikati yao, huwezi kupata umbali huo kutoka abiria na abiria.”

Hayes amesema, asilimia 40 ya viti katika ndege zake vimeondolewa huku akisisitiza kila mmoja anayepanda anapaswa kuvaa barakoa.

“Kwa kweli hatuna namna ya kwenda sawa hekana wateja wetu kwa hicho wanachokitaka,” amesema na kuongeza “kwa kweli huo ni utaratibu mpya kabisa wa abiria wetu.”

Hayes amesema, utaratibu uliopo ni kwamba, abiria yeyote anayekataa kuvaa barakoa, hatoruhusiwa kupanda kwenye ndege hizo.

“Kama ndani ya ndege kuna mtu atavua barakoa, hatoruhusiwa tena kusafiri na ndege zetu,” amesema.

Licha ya idadi ya wasafiri kuongezeka tangu idadi hiyo ilipopungua mwezi uliopita, inaelezwa bado idadi hiyo haijafikia kama ilivyokuwa mwaka 2019.

“Kuna tishio kubwa sana katika biashara hii,” amesema Hayes na kuongeza. “Nina maana kwamba, tunaingia robo ya tatu tukio na mapato 0.

“Tuna changamoto mpya katika biashara hii ambayo ni COVID-19, ni kwa namna gani abiria wetu wanaweza kuingia kwa idadi sawa ya viti na wakajiona hawapo kwenye hatari ya maambukizi?”

error: Content is protected !!