Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Heche: Polisi wameona madhara ya kukosa wapinzani bungeni
Habari za Siasa

Heche: Polisi wameona madhara ya kukosa wapinzani bungeni

John Heche
Spread the love

 

ALIYEKUWA Mbunge wa Tarime Mjini kupitia Chama cha Chadema, John Heche, amesema Askari Polisi wameona madhara ya kukosekana wabunge wa upinzani bungeni kwa kuwa wamekosa wasemaji wa changamoto zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Akizungumza katika mkutano wa hadhara leo tarehe 23 Januari 2023, Heche amedai kwamba kuna baadhi ya Polisi wamemfikisha malalamiko yao ambayo atayatoa kupitia mikutano hiyo.

Mwanasiasa huyo amedai kuwa, kutokana na changamoto wanazokabiliana nazo Polisi, hawatakubali chaguzi zijazo zichezewe.

“Kama walikuwa hawawezi kupambana na Chadema, leo Polisi wakiwa katikati wataweza kupambana? Sababu hata Polisi wameona madhara ya kukosa wabunge wa Chadema bungeni na wao wanalia na hoja zenu wameniletea nitazizungumza, kwa hiyo Polisi hawatakubali tena uchaguzi uibiwe sababu nao watakuwa kwenye moto,” amesema Heche.

Katika hatua nyingine, Heche ameitaka Serikali ihakikishe wananchi ambao ardhi zao zimechukuliwa kwa ajili ya uchimbaji madini, walipwe fidia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

Habari za Siasa

Lissu: Miaka 30 ya vyama vingi haikupambwa kwa marumaru

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Tundu...

error: Content is protected !!