Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Heche ataka mawakili vijana kuamka sakata Mpoki
Habari Mchanganyiko

Heche ataka mawakili vijana kuamka sakata Mpoki

Spread the love

MWENYEKITI wa Mawakili Vijana Tanzania kutoka Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), Edward Heche, amewataka wanachama wake kuchukua hatua pindi watakapoona sekta ya sheria na tasnia yao ya uwakili inashambuliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Heche ametoa ushauri huo leo Alhamisi, tarehe 30 Novemba 2023, akizungumza na mawakili wapya 259, kuhusu sakata la wakili mwandamizi, Mpale Mpoki, kusimamishwa uwakili kwa muda wa miezi sita, akituhumiwa kukiuka maadili ya taaluma hiyo.

Edward Heche

“Yanapotokea mambo kama haya tunapaswa tufuatilie, tuchukue hatua ikiwa pamoja na kufungua kesi za kikatiba, kupinga matumizi mabaya ya kiogisi. Tuhusike katika mageuzi ya sheria kandamizi zilizo sasa hibi ambazo zinatukuza watu wachache,” amesema Wakili Heche.

Akizungumzia sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili wakati anamtetea Wakili Boniface Mwabukusi kwenye Kamati ya Maadili ya Mawakili, Wakili Heche amesema uamuzi huo unapunguza imani ya wananchi kwa mawakili.

“Wateja wetu hawataona umuhimu wetu tena, atasema hutu nitaenda naye pale (mahakamani) lakini atasimamishwa uwakili. Ndugu zangu mawakili vijana mnaokuja kwenye tasnia hii lazima mfahamu matukio haya yanatokea sio kwa bahati mbaya, ni mashambulizi dhidi ya tasnia yetu ya uwakili. Kimsingi lazima tuweze kuihami tasnia yetu,” amesema Heche.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!