Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya Heche amvaa Ummy Mwalimu kisa bima ya afya
AfyaHabari za Siasa

Heche amvaa Ummy Mwalimu kisa bima ya afya

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, John Heche
Spread the love

 

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chadema, John Heche amemtaka Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuacha kulazimisha watu kujiunga na mpango wa bima ya afya kwa wote kwani tatizo la msingi ni upatikanaji wa huduma za afya kwa watu wote. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Pia amesema mpango wa kuwalazimisha vijana wanaojiunga vyuo vikuu kujiunga na bima ya afya ni uvunjaji wa katiba ya Tanzania.

Heche ametoa kauli hiyo leo tarehe 21 Januari, 2023 wakati akisalimia wananchi katika uzinduzi rasmi wa mikutano ya hadhara uliofanyika jijini Mwanza.

“Nipeleke ujumbe kwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu… wanaleta kitu kinaitwa bima ya afya kwa wote nataka kumwambia kuwa tatizo la watu wetu sio bima ya afya kwa wote, tatizo ni huduma ya afya kwa watu wote.

“Bima ya afya ni kitu kidogo tu, ukimpa mtu bima ya afya wakati kwenye kituo cha afya hakuna dawa, hakuna madaktari… hiyo bima ya afya haiwezi kumtibu mtu,” amesema Heche na kuongeza;

“Wanakwenda mbali wanavunja Katiba ya nchi wanasema mtoto hatokwenda chuo kikuu kama hajanunua bima yao ya afya kwa lazima. Ibara ya 11 ya katiba inasema mtu hawezi kubaguliwa kwa misingi ya kukosa mali ili asisome.

‘Tatizo la mfuko wa bima ya afya ni wizi unaofanywa na mafisadi wa CCM, unasababisha mfuko ufilisike, wao wanataka waingize watu wote kwenye mfuko wa afya wakusanye fedha nyingi waweke kwenye tenga lililotoboka. Hicho hatutokikubali,” amesema Heche.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!