January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Heche amshukia Lowassa

Mwenyekiti Mstaafu wa Bavicha, John Heche (mwenye kombati ya kaki) akiwa na Joseph Haule (mwenye mawani) kabla ya mkutano

Spread the love

MWENYEKITI mstafu wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), John Heche, amemvaa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kwamba amekuwa akitumia nyumba za ibada kujisafisha dhambi za ufisadi pamoja na kutembeza fedha kwa baadhi ya viongozi wa dini ili wamuombe agombee urais. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Heche alitoa kauli hiyo juzi, wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mbungani, Wilaya ya Nyamagana jijini hapa.

Amesema, tangu awamu ya kwanza ya Mwalimu, Julius Nyerere, Lowassa alikuwa ni mtumishi wa umma na amewahi kushika nyadhifu tofauti kitendo kinachomtia katika hukumu ya kuhusika na kashfa za ubadhilifu wa fedha za umma.

Heche alidai kuwa ni kitendo cha aibu kwa kiongozi huyo kutumia vibaya fedha zake kuhonga makundi mbalimbali yakiwemo ya wazee, vijana na viongozi wa dini ili kutengeneza njia ya kuingia Ikulu.

“Leo hii Lowassa anajisifia kujenga shule za kata ambazo zimejengwa kwa nguvu za wananchi wenyewe na sasa hata maabara zinazojengwa nchini kwa nguvu zenu atatokea fisadi mmoja ataseme amejenga yeye.

“Taifa hili limekosa viongozi ambao wana machungu na wananchi wao, sasa hivi kila kona tumezungukwa na matatizo ya kila aina, ukienda katika Wizara ya Afya hakuna madawa na katika sekta ya elimu huko sasa ndo usiseme kabisa,”amesema.

Heche ambae pia ni Mkuu wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano Chadema, amesema ni kitendo cha aibu isiyofichika kufanya kosa katika uchaguzi wa Oktoba 25, Watanzania kuchagua mgombea wa CCM.

Pia amesema Watanzania wanapaswa kuhakikisha wanakiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi huo, kwani kimeshindwa kutatua kero za wananchi na badala yake kimekuwa ni chama cha kulinda mafisadi.

Naye msanii nguli wa kizazi kipya nchini, Joseph Haule (maarufu kama Prof. Jay), ambaye ametangaza nia ya kugombe ubunge jimboni Mikumi mkoani Morogoro, amesema umefika mwisho wa CCM kutawala, kwani kaburi la kukizika

Amesema Serikali ya CCM imekuwa ikitumia fedha za umma vibaya katika kufanikisha lengo la kusahau wananchi walio waweka katika nafasi hizo, hivyo ni wakati muafaka wananchi kuachana na viongozi wa namna hiyo.

error: Content is protected !!