July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Heche aivaa serikali

Spread the love

IKIWA ni mara ya kwa Mbunge wa Tarime Vijini, John Heche (Chadema) kuhudhuria vikao vya bunge, ameanza kwa kuishambulia Serikali ya CCM kwa madai kwamba inatoa majibu ambayo hayana utafiti. Anaandika Danny Tibason, Dodoma … (endelea).

Heche ametoa kauli hiyo leo bungeni alipokuwa akiuliza maswali ya nyongeza na kudai kuwa serikali inakurupuka katika kujibu maswali lakini haifanyi utafiti.

Katika swali la nyongeza Heche amesema anasikitishwa na majibu ya serikali ambayo yanaonekana wazi kuwa hayana nia ya kuwasaidia wananchi na badala yake inatoa majibu ambayo hayana ukweli.

“Kwanza niseme kuwa nasikitishwa na majibu ya serikali ambayo hayana utafiti wa aina yoyote na wananchi hawawezi kuendelea kukubaliana na hali hiyo,” amesema Heche.

Katika swali lake la nyongeza amesema ni kwanini mgodi wa Nyamongo uliwafanyia tadhimini wananchi ambao waliposha mgodi huo lakini mpaka sasa hawajapewa fidia yao na wale ambao wamepewa fidia wamepewa fidia kidogo.

“Kwa sheria wananchi wanatakiwa kupisha mgodi kwa mita 200 na wananchi wa Nyamongo walifanya hivyo kwa ajili ya kupisha mgodi huo, na mgodi huo ulifanya tathimini kwa wananchi hao ambao walipisha mgodi kwa kuacha mashamba yao, nyumba zao huku wakiwa wanakatazwa kuendelea maeneo hayo.

“Lakini cha kushangaza ni kuona kwamba hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia zao licha ya mgodi huo kufanya tathimini na jambo la ajabu na aibu ni pale ambapo mtu mwenye shamba anaandikiwa cheki ya kulipwa kiasi cha Sh. 7273,” amesema Heche.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua ni lini wananchi hao watalipwa fidia kutokana na maeneo yao kulingana na bei ya sasa.

Aidha alitaka kujua kama fidia hiyo itaendana na usumbufu na hasara wanayopata hadi sasa.

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospiter Muhongo akijibu maswali ya Nyongeza amesema mgogoro huo ni wa miaka mingi.

“Mgogoro huo ni wa mwaka 1980 pia hata mbunge utastaafu utaacha madeni hayo kabla hayajaisha nimefanya mazungumzo mara kadhaa na viongozi juu ya tatizo hilo lakini inaonekana kuwepo kwa kitu kinachoitwa mitegesho.

“Mitegesho ni baadhi ya watu ambao wanajenga hata nyumba za thamani kubwa kwa ajili ya kutegesha kwamba watalipwa fidia lakini pia ikumbukwe kuwa jambo hilo ni la miaka mingi sana.

“Hapo Nyamongo kunahitajika kukaa zaidi ya siku tano na sasa nakuomba mbunge baada ya kumaliza twende kwa siku tano ili tuweze kukaa na wananchi na kuzungumza nao ili tuone tunafanyaje katika kutatua hali hiyo ya mgogoro huo ambao unaonekana kudumu kwa muda mrefu,” amesema Prof. Muhongo.

Naye Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medrad Kalemani amesema fidia hulipwa kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Na.4 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na.5 za mwaka 1999.

Amesema tathimini hiyo ulipwa kulingana na kipindi ambacho tathimini imefanyika.

error: Content is protected !!