November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Haya ni maajabu yake Mungu  

Hao siyo marais wa Korea Kaskazini wala Ufilipino, bali ni Cresencio Extreme (kulia) anayefanana na Rais Durtete wakati Howard X anafanana na Rais Kim.

Spread the love

AMA kwa hakika duniani ni wawili wawili. Hivi ndivyo unavyoweza kusema pale utakapokutana na Cresencio Extreme pia Howard X kwenye mitaa ya Hong Kong. Vinaripoti vyombo vya kimataifa … (endelea). 

Watu hawa wawili wamekuwa wakitikisa mitaa ya Hong Kong kutokana na namna walivyofanana na viongozi watata duniani Rodrigo Durtete, Rais wa Ufilipino na Kim Jong Un, Kiongozi wa Korea Kaskazini.

Kama utakutana na Cresencio Extreme pia Howard X mtaani, unaweza kustaajabu kuwa, imekuwaje Durtete na Kim wanatembe barabarani bila ulinzi wowote?

Watu wawili kila waliopata kuwaona, hushtuka na kudhani ni viongozi halisi kutokana na kufanana kwao.

Wamekuwa wakila pamoja, wakizungumza na kupiga picha pamoja pia wakivaa mavazi na mikato ya nywele inayoendana na viongozi halisi wa mataifa hayo mawili.

Cresencio Extreme ndiye anayefanana na Durtete wakati Howard X anafanana na Kim.

Hata walipohudhuria ibada ya Jumapili katika Kanisa la St. Joseph wakiwa na mavazi yale yanayopendwa kuvaliwa na viongozi hao halisi, walishangaza wengi.

Wakiwa mtaana viongozi hao feki walibeba bunduki na kuziinua juu wakiamini wanawasilisha hisia za viongozi wa wa mataifa hayo halisi ambapo Durtete anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu wakati Kim akipambana na Marekani kuhusu silaha zake za nyuklia.

error: Content is protected !!