MKUU wa Jeshi la Polisi IGP Camilus Wambura leo tarehe 17 Januari, 2023 amewatangazia vijana walioomba kuajiriwa na Jeshi la Polisi usaili wao utakaofanyika kuanzia tarehe 23 Januari 2023 hadi tarehe 03 Februari 2023 nchini kote. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Katika taarifa hiyo waombaji wenye elimu ya kidato cha nne waliowasilisha maombi yao kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa usaili wao utafanyika kwenye Mikoa waliyowasilisha maombi yao.
Waombaji wa Zanzibar wenye elimu ya shahada, stashahada ya juu, stashahada na astashahada usaili wao utafanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar na waombaji wenye elimu ya kidato cha nne usaili wao utafanyika kwenye Mikoa waliyowasilisha maombi yao.
Waombaji wa Tanzania Bara wenye elimu ya shahada, stashahada ya juu, stashahada na astashahada ambao walituma maombi yao kwa njia ya Mtandao, usaili wao utafanyika Jijini Dar es Salaam katika Vikosi vya Polisi vilivyoainishwa kwenye orodha ya walioitwa kwenye usaili.
Aidha usaili huo utafanyika kwa makundi mawili (2), kundi la kwanza litaanza tarehe 23 Januari 2023 hadi tarehe 27 Januari 2023 na kundi la pili litaanza tarehe 30/01/2023 hadi tarehe 03 Februari 2023.
Taarifa hiyo imesema kila mmoja atatakiwa kufika na vyeti halisi vya taaluma (academic certificates), cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha taifa (NIDA) au namba ya NIDA na cheti cha JKT au Barua ya Uthibitisho toka kwa Mkuu wa Kambi (Kwa vijana walio kwenye makambi ya JKT/JKU).
Ili kupata orodha ya vijana waliochaguliwa kufanya usaili Jijini Dar es salaam imeambatishwa pamoja INGIA HAPA.
Jamani Mimi sielewi majna ya sisi WA kidato Cha nne Dodoma mbona hatuyaoni?. Namaanisha majna ya Ajira polisi 2023
Majina ya usaili wa police dodoma
Majina ya usaili police kidato Cha nne dodoma