January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hawaza walaani kuuawa Al Nimr.

Spread the love

WAISLAM  nchini wamelaani vikali kitendo cha serikali ya Saudi Arabia cha kumuua mwanazuoni  Ayotollah Sheikh Baqir Nimr ambaye alikuwa anawatetea wanyonge na waislam nchini humo. Anaandika Aisha Amran.. (endelea)

Akisoma  tamko la kulaani kitendo hicho, Sheikh Hemed Jalala ambaye ni Kiongozi wa chuo cha kiislam  cha Hawaza Imam Swadiq, ambaye ni mmoja wa viongozi wakuu wa kiroho wa waislamu wa madhehebu ya Shia Ithna sherri Tanzania, amesema waislam nchini wamepokea kwa masikitiko kitendo cha kinyama, watu kumuua kwa kumchinja hadharani mtetezi huyo baada ya kuhukumiwa kifo na serikali ya nchi hiyo.

Amesema adhabu ya kifo aliyopewa mwanazuoni huyo ni ya kionevu kwani haendani na mafunzo ya dini ya kiislam.

“Yaani huyo Sheikh Nimr amehukumiwa baada ya kutetea haki ya waislam ikiwemo kupata  haki ya kusali mara tano kwa siku ambayo nchini Saudi Arabi hawapati nafasi hiyo, amekuwa anatetea haki ambayo serikali yake ilikuwa haiwatendei haki wananchi wake, lakini leo serikali hii ikaona njia sahihi ya kumyamazisha ni kumhukumu kifo “amesema Sheikh Jalala.

Akizungumza kwa hisia kali Sheikh Jalala  alisema inasikitisha kuona nchi kama Tanzania ambayo ina muunganiko wa dini mbali mbali lakini bado waislam wanapata haki ya kuaabudu mara tano kwa siku lakini nchi ya Saudi Arabia ambayo ni ardhi yake imetaliwa na dini hiyo waislam hawapati nafasi ya kuabudu mara tano kwa siku.

Alisema jambo hilo  linamkwaza mtume Muhamed ambaye alitaka kila mtu apewe haki ya kuabudu.

“Makosa yalitajwa na serikali ya Riyadhi juu ya Ayatollah Nimr na wenzake kwamwe hayakustahili adhabu hiyo, kumuua kiongozi mwenye wafuasi kwa kosa la kudai haki za wanyonge  ni kuchochea vurugu”amesema Sheikh Jalala.

Jalala amebainisha kuwa binadamu ni kiumbe aliye huru kutokuwa na  minyororo ya ukandamizaji na utumwa katika nyanja zote, yuko huru kutokuwa  na utumwa wa kifikra, huku akihoji ni kuwa ni kivipi karne hii ambayo uelewa juu ya masuala ya binadamu na maswala ya kielimu yameshika kasi kwanini yatokea mambo kama haya.

Vilevile Jalala ameitaka Dunia kuingilia kati vitendo vya kinyama vinavyofanywa na serikali ya Saudi Arabia kwa kunyima uhuru wa haki za kuishi pamoja na kutoa maoni.

Sheikh Baqir Nimr aliuawa tarehe 2/1/2016 baada ya kutolewa hukumu ya kunyongwa na serikali ya  Saudi Arabia kwa kosa la kushiriki kudai haki ya uhuru wa wananchi kuchagua viongozi wao kwa mfumo wa demokrasia ya wengi badala ya kuongozwa kifalme.

Kosa lingine la Nimr ni  kudai haki za binadamu ziheshimiwe kwa kuwa kuna matabaka  ndani ya nchi yananyima haki zao za msingi, pamoja na kutolewa na kuachiwa huru wafungwa wa kisaisa waliokamatwa kwa kudai mabadailiko ya kiungozi katika serikali na haki ya kuchagua viongozi wao.

error: Content is protected !!