Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hawa waripotiwe – Waziri Majaliwa 
Habari za Siasa

Hawa waripotiwe – Waziri Majaliwa 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Iringa kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa mjini Iringa. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo.
Spread the love

 

KASSIM Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania ametaka watu wanaosumbua wawekezaji kwa kuwaongezea gharama, waripotiwe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa…(endelea).

Na kwamba, wawekezaji hao pale watapoona hawahudumiwi vizuri ikiwa ni pamoja na kuongozewa kharama tofauti na uhalisia wake, watoe taarifa kwa mamlaka husika.

“Uwekezaji ni tegemeo la Taifa katika kukuza uchumi wake na kuongeza ajira, hivyo serikali inaendelea kuimarisha usimamizi wa Watumishi wa Umma wanaohusika na utoaji wa huduma kwa wawekezaji kwa lengo la kuhakikisha kuwa hawasumbuliwi.

“…na pale ambapo hawatohudumiwa vizuri ikiwemo kutozwa gharama za ziada, watoe taarifa kwa mamlaka husika,” amesema Majaliwa wakati akizindua mwongozo wa uwekezaji Mkoa wa Iringa tarehe 23 Januari 2021.

Kiongozi huo amesema, mwongozo huo umebainisha vivutio vilivyoko mkoani Iringa ikiwemo mazingira mazuri ya biashara, nguvu kazi, amani na utulivu, maliasili nyingi na soko la kutosha.

Katika uzinduzi huo amesema, serikali itaendelea kudumisha amani na utulivu kwa kuwa ni muhimu kwa wawekezaji na wananchi.

Amesema, dhamira ya serikali ni kuongeza kasi ya uwekezaji katika sekta zote na kwamba, wawekezaji wakija wawe kama marafiki na wadau muhimu kwa maendeleo ya Taifa na waungwe mkono kwenye maeneo watakayohitaji kuwekeza.

“Tuondoe vikwazo visivyo vya lazima, iwapo wamefuata taratibu zinazopaswa, sitegemei kuona wawekezaji wakikwamishwa kutekeleza miradi yao katika kila sekta na kila mkoa,” amesema na kuongeza:

“Katika ziara zangu za mikoani, nimesisitiza sana umuhimu wa watumishi wa umma kuwatumikia wananchi wote kwa usawa na bila ubaguzi.

“Aidha, nimeagiza wananchi wote na wageni wakiwemo Wawekezaji wanapofika kwenye ofisi zote za umma, wapokelewe kwa staha, wasikilizwe na kupewa huduma wanazohitaji kwa uharaka na ufanisi bila urasimu.”

Profesa Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Uwekezaji amepongeza uongozi wa Mkoa wa Iringa kwa uandaaji wa mwongozo huo.

Amewataka wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania wajipange vizuri katika kushindana kimataifa kwa kuzalisha bidhaa bora.

“Pia wajipange kuelewa mazingira ya uwekezaji hasa kufahamu sheria ambazo zinaongoza uwekezaji nchini ili waweze kuzingatia na kuzitumia ipasavyo. Kwa upande wa Serikali tutatimiza wajibu wetu kikamilifu kwa kuhakikisha kwamba mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara hapa nchini yanakuwa mazuri sana.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!