May 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Hawa ndio wababe 16 watakaokutana na Simba hatua ya makundi

Spread the love

BAADA ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba imeungana na wababe wengine 15 ambao wamefuzu kwenye hatua hiyo ya makundi mara baada ya kushinda michezo yao. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo uliopigwa jana tarehe 6 Januari, 2020 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam uliweka historia kwa timu hiyo kufuzu hatua hiyo kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu mara baada ya kufanya hivyo kwenye msimu wa mwaka 2018/19 kwa kuwafunga klabu ya Nkana FC kutoka Zambia.

Mabao ya Simba kwenye mchezo wa leo yalifungwa na Erasto Nyoni kwa njia ya penalti dakika ya 39, Shomari Kapombe dakika ya 62, John Bocco aliyetokea benchi akapachika bao la tatu dakika ya 90+1 na bao la mwisho kwenye mchezo huo likafungwa na Clotous Chama kwa njia ya penalti kwenye dakika ya 90+4.

Kwa matokeo hayo Simba anakuwa amefuzu kwa jumla ya mabao 4-1, katika michezo yote miwili kwa nyumbani na ugenini.

Mara baada ya kuibuka na ushindi huo Simba inakwenda kuungana na klabu za TP Mazembe, Zamalek SC, Kaizer Chief, Al Ahly, Mamelodi Sundowns, Esperance Tunis, Teungueth FC, CR Belouizdad, Al Merrekh, AS Vital Club, MC Alger, Wydad AC, Horoya AC na Petro Atletico.

Makundi hayo yatapangwa tarehe 8 Januari, 2020 siku ya Ijumaa jijini Cairo nchini Misri ambapo Simba atakuwa anaanzia kuifukuzia rekodi aliyoiweka kwenye msimu wa 2018/19 ya kufika hatua ya robo fainali.

Mara ya mwisho Simba kwenye hatua hiyo walipangwa kwenye kundi D, sambamba na timu za Al Ahly, AS Vital Club na JS Soura na Simba ilifanikiwa kumaliza nafasi ya pili.

error: Content is protected !!