July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Hatupandishi bei ya samaki kwa sababu ya sikukuu’

Mandhari ya soko la samaki la Feri, Magogoni jijini Dar es Salaam

Mandhari ya soko la samaki la Feri, Magogoni jijini Dar es Salaam

Spread the love

UPATIKANAJI mdogo wa samaki katika kipindi hiki cha sikukuu za Pasaka ambayo imeangukia mwezi mkali kitaalam, umesababisha bei ya kitoweo hicho kuwa ghali. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Mwenyekiti wa Soko Kuu la samaki Ferry  jijiji Dar es Salaam, Rajabu Mngoi ameliambia MwanaHALISIOnline kuwa, bei ya samaki hupanda na kushuka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, na sio kutokana na sikukuu.

Ameeleza kuwa, hakuna takwimu kamili zinazoweza kuonyesha bei kamili ya samaki, kutokana kwamba kuna mwingiliano wa kibiashara, ambapo kuna baadhi ya wauzaji hukaa nje ya soko ili kukwepa ushuru na wengine ndani ya soko na kulipa ushuru kama kawaida.

“Hawa wanaokaa nje ya soko ndio wanaharibu biashara ya wenzao, kwasababu wanunuzi wengi hupenda kununua vitu vya mafungu na sio vilivyo kwenye mpangilio maalumu.

“…hii ni kutokana na kukwepa gharama, hao ndio wanasababisha kutopatikana  kwa takwimu za bei, kwani wengine huuza kwa reja reja na jumla,” amesema Mngoi

Mngoi amesema, wafanya biashara wa ndani ya soko hawapati faida kutokana na  wauzaji  holela wa samaki kuwa wengi na hivyo kusababisha biashara hiyo kuwa ngumu.

Aliongeza kuwa wafanyabiashara wa soko hilo wapo katika mazingira hatarishi kiafya kutokana na mazingira ya ndani kuwa machafu na kusababisha soko hilo kutoa harufu mbaya muda wote.

Mngoi ametaja baadhi ya changamoto wanazozipata ni kuwa na wafanyausafi wachache, ukosefu wa ulinzi na mrundikana wa watu.

“Miundombinu kiujmla ni mibovu, kwa mfano soko la kukaangia samaki liliungua tangu mwaka 2010, lakini hadi leo ujenzi haujakamilika wala majiko banifu hayajafungwa.

“Hadi sasa utaona soko hili kubwa hapa jijini, linatakiwa kuwa na uangalizi wa kutosha. Lakini mifereji ya kupitishishia uchafu ni midogo na mibovu,” ameeleza Mngoi.

Ameitaka halmashauri ya Jiji, kuzingatia maoni ya wadau wa soko, na kutekeleza wajibu wao katika muda muafaka ili kunusuru afya za wafanyabiashara na kuendeleza soko la samaki nchini.

error: Content is protected !!