November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hatma ya pingamizi za serikali kwa Nassari kesho

Joshua Nassari

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma kesho tarehe 29 Machi 2019, itatoa uamuzi wa pingamizi tatu, zilizotolewa na serikali katika kesi ya maombi madogo ya kufungua kesi ya msingi, kutengua uamuzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri, kumfutia ubunge wa Joshua Nassari (Chadema), katika Jimbo la Arumeru  Mashariki. Anaripoti Danson Kaijage … (endelea).

Kwa mujibu wa Jaji Latifa Mansoor anayesikiliza kesi hiyo namba 22 ya mwaka 2019, amesema mahakama inatarajiwa kusikilizwa pingamizi za serikali tarehe 29 Machi 2019 ambapo hata hivyo, hakutaja pingamizi hizo.

Amesema, uamuzi huo umekuja baada mahakama kupokea pingamizi ziliyotolewa na upande wa serikali ukiwakilishwa na mawakili wawili ambao ni Alisia Mbuya na Masunga Kawahanda.

Tarehe 20 Machi 2019 mahakama ilitoa siku saba kwa upande wa serikali ambao ni Spika wa Bunge la Jamhuri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupeleka kiapo kinzani cha maombi hayo.

error: Content is protected !!