September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Hatma ya Kitilya na wenzake Mahakama Kuu kesho

Spread the love

MOSES Mzuna, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Dar es Salaam, amesema kesho hatima ya kusikiliza kesi ya inayowakabili Harry Kitilya, Shose Sinare na Sioi Solomon katika mahakama kuu itajulikana, anaandika Faki Sosi.

Kitiliya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji na Sioi, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tawi la Tanzania.

Alex Mngongolwa Wakili wa upande wa utetezi ametoa hoja kuwa hakuna sababu za kusikiliza kwa rufaa hiyo kutokana na kesi bado ipo haijafutwa yote isipokuwa imefutwa shitaka moja.

Timon Vitalis Wakili wa Serikali amedai kuwa Emilius Mchauru Hakimu Mkazi Kisutu kwa kutoa maamuzi bila kuzingatia matakwa ya sheria.

Timon ameeleza kuwa Hakimu Mchauru alikosea aliposema kuwa hati yetu ina dosari kwani hati yetu haina dosari yoyote kisheria.

Ameleeza kuwa bado sheria ipo wazi kwa upande wa waandesha mashitaka kurekebisha hati ya mashitaka kabla ya kuleta mashahidi au baada.

Moses Mzuna, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam amesema kuwa, Mahakama imesikiliza hoja za pande zote mbili kesho atatoa maamuzi aidha itasikilizwa rufaa ya kesi hiyo au kutosikiliza.

error: Content is protected !!