May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hatma wateja FBME bado njia panda

Spread the love

 

WATEJA wa Benki ya Biashara ya FBME, wameshindwa kulipwa fedha zao kwa haraka kutokana na kutokukamilika kwa taratibu za kisheria. Anaripoti Jemima Samwel DMC … (endelea).

Ni kauli ya Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango aliyoitoa leo tarehe 21 Aprili 2021, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali Catherine Magige, Mbunge wa Viti Maalumu aliyehoji hatma ya baadhi ya wateja wa benki hiyo.

Benki ya FBME ilipokonywa leseni ya uendeshaji na BoT Julai 2014 sambamba na kuikwekwa chini ya ufilisi, ikituhumiwa kujihusisha na utakatishaji fedha.

“Iliyokuwa Benki ya FBME sasa ni zaidi miaka minne tangu BoT (Benki Kuu) waifunge, wananchi wa Arusha na sehemu mbalimbali waliokuwa na akaunti katika benki hiyo, hadi leo hawajui hatma ya fedha zao. Nini kauli ya serikali?” amehoji.

Dk. Nchemba amesema, “taratibu za kisheria huwa zinachukua muda, hicho ndicho kimechelewesha sasa ni  lini utakamilika, nakumbuka utaratibu ulikuwa uanendelea na ulikuwa katika hatua nzuri, tutakapokuwa tuememaliza bungeni nitapata taarifa lini litakuwa limekamilika sababu zoezi lilikuwa linaendelea.”

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Amesema, wateja ambao hadi sasa hawajalipwa fedha zao, ni wale ambao wanasubiri taratibu za ufilisi zikamilike ikiwemo kuuzwa kwa mali za benki hiyo, kwa ajili ya kutafuta fedha za kuwarudishia.

“Ni kweli kulikuwepo zoezi la kuichukua iliyokuwa benki ya FBME na  ikilichochelewesha ni ule utaratibu ambao ni wa kawaida, unapokabidhi kwa mufilisi kwa hatua zile kwamba  unatoa kile cha kwanza ambacho kipo kisheria kwa wale waliokuwa na akiba zisizozidi kiwango kilichowekwa kisheria,” amesema Dk. Nchemba.

“…lakini kwa wale ambao viwango vyao vilikuwa zaidi ya kiwango kinachogawanywa kwa awamu ya kwanza, huwa lazima zoezi la mufilisi likamilike ambalo linahusu uhakiki wa mali zilizopo zikusanywe, ziuzwe na zigeuke kuwa fedha ndipo watu waweze kugawanya.”

error: Content is protected !!