Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Hatma kesi ya wadhamini ‘kumtosa’ Lissu kujulikana Julai 5
Habari MchanganyikoTangulizi

Hatma kesi ya wadhamini ‘kumtosa’ Lissu kujulikana Julai 5

Spread the love

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirisha kutoa uamuzi wa pingamizi la Jamhuri dhidi ya kesi Na. 2/2020, iliyofunguliwa na wadhamini wa Tundu Lissu, ya kutaka kujitoa kwenye udhamini wa mwanasiasa huyo, katika kesi ya uchochezi Na. 208/2016. Anaripoti Jemima Samwel, DMC … (endelea).

Wadhamini wa Makamu Mwenyekiti huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, ni Meneja wa Kampuni ya uchapishaji Magezeti ya Hali Halisi Publishers, Robert Katula na Ibrahim Ahmed, ambaye ni mfanyakazi wa kampuni hiyo.

Leo Jumatatu tarehe 7 Juni 2021, mahakama hiyo chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, ilipanga kutoa uamuzi wa pingamizi hilo, lakini ilishindikana kutokana na uamuzi huo kutokuwa tayari.

Hivyo, Hakimu Simba amepanga tarehe 5 Julai 2021, kuwa siku ya kutolewa uamuzi juu ya pingamizi hilo, ambao utaamua kama kesi hiyo ya kujitoa udhamini iendelee au isiendelee.

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema

Upande wa Jamhuri kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, uliweka pingamizi la kuzuia wadhamini hao kujitoa, mwezi Julai 2020, kwa madai kwamba kesi ya msingi haijafika mwisho.

Mbali na Lissu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uchochezi ya 2016, ni Mhariri Mkuu wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina. Mwandishi Mwandamizi wa gazeti hilo, Jabir Idrissa na Meneja wa Kampuni ya Uchapishaji ya Flint, Ismail Mahboob.

Washtakiwa hao wanashtakiwa kwa makosa ya kufanya uchochezi kupitia gazeti hilo, wanayodaiwa kufanya 2016, kwa kuchapisha habari yenye kichwa ‘Machafuko yaja Z’bar’.

Wadhamini wa Lissu waliamua kufungua kesi mahakamani hapo, kuomba kujitoa katika udhamini wa Lissu kwenye kesi hiyo.

Kwa madai kwamba hawana uwezo wa kumpeleka Mahakamani mahtakiwa huyo, ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni nchini Ubelgiji. Pia, wanadai hawana uwezo wa kuwasilisha mahakamani hapo, taarifa za matibabu ya Lissu.

Hatua ya wadhamini hao kutaka kujitoa, ilichukuliwa takribani miaka minne. Tangu kesi hiyo kufunguliwa, baada ya Lissu kuwa nje ya nchi kwa muda mrefu na kusababisha wadhamini hao kushindwa kumfikisha mahakamani.

Kutoka kushoto, Jabir Idrissa, Mhariri wa Mawio, Simon Mkina, Mhariri na Mmiliki wa gazeti la Mawio na Tundu Lissu walipokuwa mahakamani katika kesi ya uchochezi kupitia gazeti la Mawio

Mwaka 2018, Lissu aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chadema, alipelekwa nchini Ubelgiji kwa ajili ya kupata matibabu, baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana, akiwa nyumbani kwake Area D jijini Dodoma, terehe 7 Septemba 2017.

Lissu alisafirishwa kuelekea Ubelgiji, akitokea jijini Nairobi nchini Kenya, alikopelekwa Septemba 2017, kwa ajili ya kupata matibabu ya awali, baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.

Lissu aliishi Ubelgiji hadi Julai 2020, aliporejea nchini kwa ajili ya kushiriki Uchaguzi Mkuu, ambapo alikuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema, akichuana vikali na aliyekuwa mgombea wa CCM, Hayati John Magufuli.

Lakini Lissu aliangukia pua kwenye kinyan’ganyiro hicho, baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kumtangaza Magufuli mshindi.

Novemba 2020, siku kadhaa baada ya matokeo ya uchaguzi huo kutangazwa, Lissu alirejea tena Ubelgiji akidai kwamba usalama wake nchini Tanzania, ulikuwa hatarini. Kufuatia kupokea jumbe za vitisho.

Katika nyakati tofauti, Lissu alidai kwamba anapokea vitisho kutoka kwa watu wasiojuliakana, lakini vyombo vya dola vilikanusha tuhuma hizo na kumtaka arejee nchini, kwani viko tayari kumpatia ulinzi yeye na familia yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 120 za DMDP zaibadilisha Ilala, wananchi watoa ya moyoni

Spread the loveJUMLA ya Sh bilioni 120.7 zimetumiwa na Halmshauri ya Jiji...

error: Content is protected !!