Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Hatimaye Lema awasili Tanzania, akabidhiwa biblia na wazee wa Chadema
Habari za Siasa

Hatimaye Lema awasili Tanzania, akabidhiwa biblia na wazee wa Chadema

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, amewasili nchini akitokea Canada, alikokuwa akiishi tangu 2020 baada ya kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa mwaka huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Lema amewasili Tanzania mchana wa leo tarehe 1 Machi 2023, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambapo anatarajiwa kusafiri hadi jijini Arusha, kwa ajili ya kushiriki mkutano wa hadhara wa Chadema.

Mwanasiasa huyo machachari nchini, amepokewa na umati wa watu waliofika uwanjani hapo, ambao walikuwa wamevaa sare za Chadema.

Baada ya kuwasili uwanjani hapo baadhi ya wazee ambao ni wafuasi wa Chadema, walimkabidhi biblia ya lugha ya kimachame, kama ishara ya kumpokea.

Mwakilishi wa wazee hao alimkabidhi biblia hiyo, huku akimkaribisha nyumbani baada ya kuishi ughaibuni nchini Canada kwa miaka zaidi ya miwili.

Lema ni miongoni mwa wanasiasa wa Tanzania waliokimbia nchi baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2020, kwa madai ya kupokea vitisho vya kiusalama. Viongozi wengine waliokimbia nchi kwa madai hayo walikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu na Ezekiel Wenje na wote wamerejea Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!