Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hati ya dharura: Zitto aeleza hofu
Habari za SiasaTangulizi

Hati ya dharura: Zitto aeleza hofu

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo
Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeupinga Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Makampuni, kikisema ni hatari kwa masuala ya uwekezaji nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza na wanahabari tarehe 24 Juni 2019 Jijini Dar es Salaam, Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe amesema kifungu 400A cha muswada huo, kinampa mamlaka Msajili wa Kampuni kufuta kampuni “wakati wowote anaotaka.”

Zitto ameeleza kuwa iwapo muswada huo utapitishwa na Bunge na kuwa sheria, kampuni zitakuwa hatarini kufungwa ovyo na serikali, kama mmiliki au kiongozi wake atabainika kufanya kosa.

Amesema kwamba, mamlaka hayo yanayopendekezwa na serikali kuyamiliki Msajili, ni tofauti na yaliyomo kwenye sheria iliyopo ambayo hairuhusu kampuni kufungwa kutokana na makosa ya mmiliki au kiongozi wake.

Zitto amesema, muswada huo ni hatari kwa uwekezaji kwa sababu anaamini hakuna mwekezaji atakayekuwa tayari kuwekeza katika nchi ambayo anajua serikali ina mamlaka ya kuifunga kampuni wakati wowote pasipo mchakato wa sheria kufuatwa.

“Hili ni jambo la hatari sana, huu muswada tayari wabunge tumepewa, mjadala kwenye kamati husika umeanza lakini hatuoni mijadala kwenye jamii kwa sheria mbaya kama hii. Kampuni zikifungwa ovyo ovyo watu watakosa ajira, haya ni mambo ambayo hayapaswi kutokea kwenye nchi yetu.

“Tunakwenda kuunda kitu tofauti kabisa, tutakuwa peke yetu dunia wenye kitu cha namna hii, ndio mapendekezo ambayo serikali inayaleta, ni ya hatari kwa uwekezaji nchini na hakuna mtu atakayekuja kuweka fedha zake kwenye mazingira kama haya yanayojengwa katika nchi yetu. Iwapo serikali ina mamlaka wakati wowote kuifuta kampuni yake, huwezi kupata mwekezaji,” amesema.

Badala yake, Zitto ameiomba serikali kutafuta mbinu nyingine za kutatua changamoto zinazodhoofisha uimara wa makampuni nchini, bila ya kuathiri shughuli zao.

Pia ametoa wito kwa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini pamoja na wafanyabiashara wote nchini kupaza sauti zao kuupinga muswada huo, vinginevyo watakuja kuwajibika kwa kulazimika kukabiliana na mkono katili wa serikali.

“Nawaomba TPSF, shirikisho la watu wenye viwanda na wafanyabiashara wengine wote watambue sasa serikali wakati wowote ikitaka inaweza ikafuta kampuni yoyote, hatua ambayo inakwenda kinyume kabisa na viwango vya kiutendaji vya kimataifa,” amesema Zitto.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!