September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hashimu, Lutembeka warudishwa Baraza la Wazee Chadema

Hashimu Juma Issa, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema

Spread the love

HASHIMU Juma Issa, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Wakati huo huo, Roderick Lutembeka ameteuliwa tena kuwa Katibu wa Baraza hilo, katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Kabla ya uchaguzi huo, Lutembeka alikuwa Katibu wa baraza hilo, na Hashimu alikuwa mwenyekiti.

Taarifa ya kuchaguliwa kwa viongozi hao, imetolewa leo tarehe 12 Desemba 2019 na Chadema katika ukurasa wake wa Twitter.

Hivi karibuni Chadema imefanya uchaguzi wa viongozi wa mabaraza yake, ambapo matokeo ya uchaguzi wa Baraza lale la Vijana  (BAVICHA) yameshatangazwa.

Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) bado halijafanya uchaguzi wake.

error: Content is protected !!